Saturday, March 20, 2021
Nimeridhishwa Na Maandalizi Ya Ibada Na Heshima Za Mwisho Kwa JPM Uwanja Wa Uhuru- Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam na mikoa jirani leo Machi 20 na kesho Machi 21, 2021 watapata fursa ya kushiriki Ibada ya kumwombea Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kutoa heshima za mwisho katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kukagua maandalizi ya tukio jana Ijumaa, Machi 19, 2021, Mheshimiwa Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi yanayofanywa chini ya usimamizi wa Kamati ya Kitaifa ya Maafa ambayo yeye mwenyewe ndiye Mwenyekiti wake akishirikiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.
Mheshimiwa Majaliwa amesema Ibada hiyo itatanguliwa na ibada nyingine itakayofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es salaam ambako marehemu amekuwa akiabudu wakati wote alioishi Dar es salaam.
Amesema wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salam na mikoa jirani wanaotamani kumuaga aliyekuwa rais wao mpendwa ambaye amefanya mambo mengi na makubwa jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla wafike uwanja wa Uhuru kuanzi saa 11 alfajiri amabapo watapokelewa na kuonyeshwa mahali pa kukaa.
Mheshimiwa Majaliwa amesema fursa ya kutoa heshima za mwisho itatolewa hadi saa 12 jioni na endapo itaonekana kuwa bado wapo watu wengi wanaotamani kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao muda utaongezwa hadi watakapomalizika.
Amesema Machi 22, 2021 mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Dodoma ambako maombolezo ya kitaifa yatafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri na waombolezaji wa mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani pamoja na wambolezaji kutoka nje ya nchi watapata fursa ya kushiriki na kutoa heashima za mwisho.
Machi 23, 2021 asubuhi mwili utasafirishwa kwa ndege kutoka Dodoma kwenda Mwanza ambako shughuli za maombolezo zitafanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba na wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Mheshimiwa Majaliwa amesema, Machi 24 mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Chato ambako wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa jirani watapata fursa ya kumuaga marehemu. Amesema Machi 25 mapema asubuhi itafanyika Ibada nyumbani kwa marehemu Chato ikifuatiwa na mazishi.
Awali, Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Ikulu Ndogo jijini Dar es salam kutoa pole kwa Mjane wa Marehemu Mama Janet Magufuli pamoja na familia na baadae alikwenda kwenye Viwanja vya Karimjee kutia saini kitabu cha maombolezo.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema kuwa anafarijika kuona kwamba siku zote umekuwepo ushirikiano wa dhati kati Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika nyakati za shinda na raha.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumk...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospita...
-
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mjasiriamali Faiza Ally ameweka wazi hisia zake na kusema kuwa anatamani sana kuona msanii wa Bongo Flev...
-
UNAPOTAJA jina la mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' kutoka Tanzania, akili za wengi zinakimbilia kwe...
-
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari ikiwemo mafuriko. ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Geneva, Switzerland /AFP /.More than 100 groups urged the International Labour Organization to stop taking money from tobacco companies as t...