Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.
Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye kikombe na umgorogee na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi, kitu cha kujiuliza je mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu.
Mtu huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema sifanyi biashara yeyote ile mi nipo tu, ukimuuliza kwanini haufanyi biashara yeyote tatizo nini? Utamsikia anakujibu tatizo mtaji huku akiamini kuwa mataji pekee katika biashara ni fedha. Ndugu msomaji wa makala hii hata uwe na fedha kiasi gani kama huna wazo kwa ajili ya matumizi ya fedha, hata ukipewa milioni mia moja leo hizo pesa zitaisha utajikuta mwisho wa siku huna hata mia mbovu. Watu wengi tunatazama mitaji kama fedha peke yake ukitazama katika msingi huo utazidi kulamu mpaka mwisho huku maisha yakiendelea kuwa magaumu.
Ngoja nikuibie siri mtaji unaweza ukaupata kwa kutumia ujuzi pamoja nguvu ulizonazo ili kutengeneza bidhaa au huduma zitazokufanya upate fedha. Kwa mfano Wewe mwenye elimu juu tekinologia ya habari na mawasiliano unaweza ukabili ujuzi wako kuwa bidhaa kwa kuwa fundi wa computer na kutengeza progamu mbalimbali. Swali la kujiuliza unaweza vipi kubadili ujuzi ulio nao kuwa bidhaa au huduma hapo ndipo wengi tunapofeli kwa sababu ni wavivu wa kufikiri.
Naendelea kumchambua binadamu ili uone ni jinsi gani tulivokuwa na tabia za lawama. Binadamu huyo huyo utamkuta anaishi mazingira machafu ambayo yatasababisha muda wowote magonjwa ya mlipuko kutokea, ukimfuta bianadamu huyo na kumuuliza unafikiri ni kwanini mazingira haya ni machafu, utamsikia jibu atakalokupa atakwambia tatizo ni serikali, binadamu huyohuyo utamkuta hana ajira ila ukimuuliza kwanini hauna ajira? Atakujibu tatizo ni serikali.
Kuna msanini mmoja wa hip-hop anaitwa nikki mbishi aliwahi imba kwenye wimbo huku akiuliza serikali ni nini? Maana imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila kitu. Ndugu msomaji wa makala haya nakusihi na kukushauri pia kwa kile ambacho unaweza kukifanya usisubiri serikali ndio ukifanyie, kama unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako fanya usisubiri kuambiwa, maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa wanasubiri kuambiwa fanya hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya mafanikio kwa upande wako yatakuja kwa asilimia chache sana.
Kitu cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na msingi wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata Yule unayemlalamikia hakusikii na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu kwa moyo mmoja bila kusubiri mtu Fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke usemi huu "kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari''
Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini upo hapo ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa Kiswahili unasema kila binadamu ni mchunga ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma makala hii endapo utaulizwa Swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha uone una thamani gani mbele ya watu wengine?
Na: Benson Chonya
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...