MWANAMUZIKI Mmarekani T.I. (jina lake halisi ni Clifford Joseph Harris Jr) na mkewe wamevunja ukimya, wameibuka na kukanusha tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizotolewa na wanawake zaidi ya 25 wiki hii.
Rapa huyo ametumia njia ya video kuzungumzia suala hilo, amesema tuhuma hizo ni uongo na hazina ukweli wowote. "Kwa nguvu zote na hekima tunakanusha tuhuma hizi za kipuuzi zilizotolewa na watu wasiofahamika." yalisomeka maelezo kwenye video hiyo yenye dakika nane.
T.I. aliendelea kusema kwamba ilikuwa ngumu kuweza kukaa kimya kufuatia tuhuma hizi ambazo pia zinamchafua na mkewe, Tiny Harris. Anaamini amechafuliwa (defamed) kwa sababu wanaomtuhumu hawajafungua shauri lolote mahakamani.
"Hatujawahi kumlazimisha mtu yeyote, hatujawahi kumhusisha mtu yeyote kwenye masuala ya kingono, hatujawahi kumteka mtu yeyote pasina ridhaa yake. Hatujawahi kusafirisha chochote, yaani kinachohusu biashara ya ngono," alisema T.I. na kukanusha pia tuhuma za kubaka: "Sijawahi kumbaka mtu yeyote, kamwe sijawahi kumbaka yeyote."
Source