Baba mzazi wa rapa Onika Tanya Maraj maarufu Nicki minaj, Mzee Robert Maraj (64) amefariki dunia akiwa hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ajali ya gari huko jijini New York, Marekani.
Kwa Mujibu wa mtandao wa TMZ, Polisi wa Kaunti ya Nassau wanasema #RobertMaraj alikuwa akitembea kati ya Barabara ya Roslyn na Raff Avenue Ijumaa jioni (Februari 12) majira ya jioni, ndipo alipogongwa na gari lililokuwa likielekea Upande wa kaskazini.
Polisi wanasema, mara baada ya ajali hiyo kutokea, Dereva alikimbia eneo hilo na bado anatafutwa. Baba wa #NickiMinaj (miaka 64) alipelekwa katika hospitali ya eneo hilo akiwa katika hali mbaya na kupelekea kifo chake.
Hata hivyo, Nicki Minaj bado hajazungumza juu ya kifo cha baba yake haswa kwenye mitandao ya kijamii. Uhusiano wao umekuwa na shida kwa miaka mingi, kwa hivyo haijulikani hali yao ilikuwaje mpaka kifo cha Baba yake kinatokea.
Mwaka 2010, Nicki Minaj aliweka wazi kuwa Baba yake, alikuwa anakunywa sana pombe na alikuwa akitumia dawa za kulevya, na kuna siku almanusura amuue mama yake mara baada ya kusababisha nyumba aliyokuwepo mama yake kuwaka moto.