Tuesday, February 2, 2021
Rais Magufuji amuapisha Zepharine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani
Rais Dkt. John Magufuli amemuapisha Zepharine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania ikiwa ni siku moja baada ya kumpandisha cheo ambapo awali alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma.
Akizungumza muda mfupi baada ya kumuapisha Jaji Galeba leo, Rais Magufuli amesema kuwa miongoni mwa mambo yaliyosababisha akampandisha cheo ni pamoja na uthubutu wake wa kutoa hukumu ya kesi kwa lugha ya Kiswahili.
Rais Magufuli amesema madai kuwa lugha ya Kiswahili haiwezi kutumika mahakamani kwa sababu haina misamiati ya kutosha hayana tija kwa sababu hakuna lugha yoyote duniani ambayo inajitosheleza.
"… tunashindwa kukitumia Kiswahili kwa sababu ya kukosa utashi na ujasiri. Lakini pia ni ishara ya kuendelea kwa kasumba fulani ya kupenda vitu vya nje na kudharau vya ndani," ameeleza Rais Magufuli na kuongeza kuwa alimteua Jaji Galeba kwa sababu amekuwa na udhubutu na ujasiri wa kuandika hukumu kwa Kiswahili.
Rais amesema kuwa kushindwa kuitumia lugha hiyo kwenye masuala ya kimahakama na kisheria siyo tu kunawanyima haki wananchi, bali pia kuwaongezea gharama kupitia ukalimani wa kutafsiri hukumu na mienendo ya kesi.
Kwa upande wa Jaji Galeba amemshukuru Rais kwa nafasi hiyo ya juu zaidi katika idara ya mahakama na amemuahidi kutenda kazi kwa bidii na kutenda haki kwa wananchi.
"Sina maneno ya kueleza namna nimepokea hii nafasi, labda niseme tu kwa ufupi kwamba nakuahidi kutumikia wananchi wa nchi hii kwa kutenda haki vile ambavyo Mungu anataka tutende haki huku duniani," amesema Jaji Galeba.
Jaji Galeba alitoa hukumu hiyo katika kesi ya North Mara Gold Mine Ltd dhidi ya Gerald Nzumbi katika kesi ya Mapitio Na. 23 ya Mwaka 2020.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...