Monday, February 1, 2021

Picha : EWURA YAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje (kulia) akizungumza kwenye mafunzo kuhusu EWURA kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendesha mafunzo kwa Waandishi wa habari Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuwafahamisha waandishi wa habari kuhusu kazi,wajibu na mafanikio ya EWURA katika udhibiti wa huduma za Nishati na Maji.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Jumatatu Februari 1,2021 na kukutanisha waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Geita na Simiyu katika ukumbi wa Gold Crest Jijini Mwanza ambapo wamepata fursa ya kufahamishwa kuhusu kuanzishwa kwa EWURA, sekta inazozitawala, muundo wake, mafanikio na changamoto zake.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje amesema waandishi wa habari ni wadau wakubwa wa EWURA katika utendaji wao wa kazi na kwamba wanafanya kazi kwa uwazi na mara nyingi wamekuwa tayari kutoa ufafanuzi kwa jambo lolote lile ambalo waandishi wa habari wanahitaji ili kuihabarisha na kuielimisha jamii.

Chibulunje amesema EWURA itaendelea kutoa ushauri kwa serikali katika kuandaa sera,sheria na kanuni zitakazowezesha kukua kwa sekta za nishati na maji na kuendelea kusimamia watoaa huduma ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora kwa manufaa ya taifa.

Aidha amesema EWURA imesaidia kuzuia mfumko wa bei, kuimarisha mamlaka za maji nchini na kukuza umeme binafsi na kwamba itaendelea kuzingatia misingi mikuu sita ya utawala bora katika maamuzi ya udhibiti ambayo ni weledi, uwajibikaji, utabirikaji, ushirikishaji, uwazi na kufuata sheria.
 Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina amewaomba waandishi wa habari kuendeleza ushirikiano walionao kwa EWURA nao wataendelea kutoa ushirikiano.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza, Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa kuandaa mafunzo hayo na kuahidi kuwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wataendelea kushirikiana na EWURA.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa leo Jumatatu, Februari 1,2021. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa leo Jumatatu, Februari 1,2021. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina, katikati ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo.
Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje akiwasilisha mada kuhusu kuanzishwa kwa EWURA,sekta inazozitawala, muundo wake,mafanikio na changamoto zake.

Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina, katikati ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari  mkoa wa Mwanza, Edwin Soko akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Geita na Simiyu wakiwa katika ukumbi wa Gold Crest Jijini Mwanza 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...