Wednesday, February 3, 2021

Mbunge Mageni adai kuna ufisadi kwenye halmashauri


 Mbunge wa Sumve (CCM),  Kasalali Mageni ameitaka Serikali kushughulika na ufisadi katika ngazi ya halmashauri na Wilaya alikodai kuwa bado kuna shida.


Mageni ameeleza hayo leo Jumatano Februari 3,  2021 katika mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli ya ufunguzi wa Bunge la 12.


Amesema katika ngazi za juu Serikali imefanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini katika maeneo ya chini akitolea mfano halmashauri na Wilaya kazi kubwa inahitajika.


Amebainisha kuwa kwenye halmashauri na Wilaya fedha nyingi za matumizi zinapelekwa lakini hazitumiki inavyotakiwa na kwamba bado kuna miradi hewa, usimamizi mbovu wa fedha na fedha nyingi kupotea.


"Hata ubora wa majengo na miradi inayosimamiwa na halmashauri haujafikia viwango vinavyotakiwa. Tamisemi inatakiwa kuangalia halmashauri kwa jicho la pili," amesema

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...