Sunday, February 14, 2021

Malori ya Mafuta yateketea Katika Moto Mpakani Mwa Iran na Afghanistan

 


Malori kadhaa ya kubeba gesi na mafuta yaliyokuwa yamebeba mafuta ya thamani ya mamilioni ya dola yaliteketea hapo jana Jumamosi na kusababisha moto mkubwa katika eneo kubwa la kibiashara katika mpaka kati ya Afghanistan na Iran. 

Moto huo ulizuka majira ya mchana katika bandari ya Islam Qala umbali wa kilomoita 120 kutoka mji wa Herat na kuteketeza malori hayo yaliokuwa yameegeshwa karibu na hapo baada ya kuvuka mpaka. Mkuu wa chama cha biashara mjini Herat Younus Qazi, amesema kulikuwa na malori kati ya 200-300 katika eneo hilo na wakaweza kuokoa baadhi lakini mengi yaliteketea. 

Ameongeza kuwa moto huo ulikuwa mkubwa sana na hakuna mtu angeweza kufika hata kilomita moja karibu nao. Ibrahim Mohammadi, mkuu wa huduma za magari ya kusafirisha wagonjwa katika mkoa wa Herat amesema kuwa kiasi ya watu wasiopungu 17 wamepelekwa hospitalini wengi wao wakiwa na majeraha mabaya ya moto.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...