Tuesday, February 9, 2021

Jeshi la Myanmar lapiga marufuku mikusanyiko katika miji mingi


Maafisa nchini Myanmar wameongeza idadi ya maeneo yaliyopigwa marufuku watu kufika nchini humo.

 Hatua hiyo sasa inamaanisha maeneo mengi nchini humo hayaruhusiwi watu kufika baada ya waandamanaji kukabiliana na polisi katika miji chungunzima ya nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia.

 Tangazo hilo limetolewa na kitengo cha habari cha kijeshi.

 Katika maeneo hayo mikusanyiko ya watu zaidi ya watano hairuhusiwi na amri ya kutotoka nje imewekwa ikiwemo katika mji wa kibiashara wa Yangon, mji mkuu Naypitaw pamoja na miji mingine katika majimbo kadhaa ya nchi hiyo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...