Thursday, February 25, 2021

Jamii imetakiwa kuwathamini na kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu


 JAMII imetakiwa kuwathamini na kuwajali watoto waliofiliwa na wazazi wao na wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao waweze kupata mahitaji yao ya msingi ikiwemo elimu, makaazi na malazi kama wanavyopata wengine.

Hayo ameyaeleza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi na Mbunge wa Jimbo la  Uzini Khamis Hamza Chilo huko Skuli ya Kidimni wakati wa kutoa msaada wa nguo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu waliomo ndani ya Jimbo la Uzini uliofadhiliwa na taasisi ya Noah Development Services Assocition kutoka nchini China.

Amesema lengo la msaada huo ni kuona watoto hao wanaishi katika mazingira bora na kuvaa vizuri ili wasijiskie tofauti kati yao na watoto wengine katika jamii, hivyo amewaomba wafadhili kutoa misaada ya hali na mali kila hali itapokaporuhusu.

''Niwaombe ndugu zangu mliotupa tupa msaada huu msichoke kuendelea kutupatia misaada mengine muhimu kila hali zenu zitavyoruhusu na tunawakaribisha taasisi nyengine kuja kutusaidia ili hawa watoto wetu wapate furaha katika utafutaji wao wa elimu'' alisema Naibu Waziri huyo.

Nae Mwakilishi wa Jimbo hilo Haji Shaaban Waziri ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo walioutoa na kuahidi kuwa msaada huo utatumika na kuwafikia walengwa wailokusudiwa ikiwa ni pamoja na watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wanaoishi katika Jimbo hilo.

Aidha amewataka wazee waliokabidhiwa nguo hizo kwa niaba ya watoto hao kuhakisha nguo hizo wanawapatia walengwa waliokusudiwa pamoja na kuzitunza ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Mkurungenzi wa taasisi ya Noah Development Services Association Bi Kwan il Park ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaruhusu na kushirikiana nao katika miradi ya kimaendeleo  ikiwemo Skuli , Vituo vya Afya na huduma za maji safi na salama  kwa vitongoji na vijiji vilivyomo mkoawa Kusini.

Aidha msaada huo wa nguo uliotolewa na taasisi hiyo una thamani ya shilingi million saba na umetolewa kwa watoto  mia moja hamsini ambao miongoni mwao ni mayatima na wanaoishi katika mazingira magumu wa Jimb

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...