Wednesday, January 6, 2021
WAZIRI JAFO AIPA TANO MISUNGWI UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA
Na Atley Kuni, Mwanza
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo ameoneshwa kufurahishwa na kupongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungi mkoani Mwanza kwa ubora wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Mpaka sasa utekelezaji wa ujenzi huo wamekamilisha majengo ya maabara pamoja na jengo la wagonjwa wanje (OPD), baada yakupokea Sh milioni 500 katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo, Waziri Jafo, amesema: " miongoni mwa halmashauri zinazo nishawishi kwenda kuomba fedha zingine kwa Mhe. Rais John Pombe Magufuli ni pamoja na Halmashauri hii ya Misungwi.
"Ndugu zangu mimi, niwapongeze kwa kazi kubwa mlio ifanya, haihitaji kuwa na darubini kubaini ubora wa majengo haya, ukiangalia milango, Vigae, vioo nk. mliyotumia lakini hata uimara wa maeneo mbalimbali hii inatia hamasa sana, pamoja na kwamba hamkuwepo katika bajeti iliyopita lakini mmeitendea haki fedha iliyoletwa, hongereni sana."
Awali akitoa taarifa ya ujenzi huo, Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo, Kisena Mabula, amesema kukamilika kwa hospitali hiyo, itakuwa na uwezo wa kuwahudumia watu wapatao 462, 855 wa wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya Mhe. Waziri Jafo, inaonesha hadi kukamilika kwa Hospitali hiyo itatumia kiasi cha Sh 2, 076 468, 848, ambapo katika hatua za awali halmashauri ilipokea kiasi cha Sh milioni 500 kutoka Serikali kuu, zilizo tumika kukamilisha ujenzi wa jengo la maabara pamoja na jengo la wagonjwa wanje (OPD).
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela, alimpongeza Mhe. Waziri Jafo kwa ziara yake katika Mkoa huo, huku akimhakikishia kuwa wataendelea kusimamia miradi yote kwa umakini mkubwa kadri watakavyokuwa wanaipokea.
" Nikuhakikishie mheshimiwa waziri (Jafo) kuwa tutasimiamia kwa umakini miradi yote itakakayokuwa inatekelezwa katika mkoa wetu lakini pia tunatingatia maelekezo ya viongozi wote wa juu akiwepo Mhe. Rais mwenyewe."
Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni moja kati ya Hospitali 97 zinazo endelea kujengwa nchi nzima
Awamu ya kwanza ya unejzu wa hospitali za wilaya ilijumuisha kujenga hospitali 67 na katika awamu ya pili inajumuisha ujenzi wa hospitali za wilaya 28 ambazo tayari ujenzi wake umanza ikiwa ni azima ya Serikali ya awamu ya tano kusogeza huduma karibu na wananchi.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
