Sunday, January 3, 2021

Mume apewa talaka kwa kujifanya kiziwi kwa miaka 62 akwepa kusikia maneno ya mkewe


Mwanaume mmoja kutoka Marekani amepewa talaka na mke wake mara baada ya kuigiza kuwa kiziwi kwa muda wa miaka 62 akidai kujizuia kumsikiliza mkewe.

Barry Dawson mwenye umri wa miaka 84 hakuwahi kuongea neno lolote mbele ya mke wake Dorothy mwenye umri wa miaka 80 kwa kipindi chote walichoishi pamoja akidai kuwa amefanya hivyo kuilinda ndoa yake iliyodumu kwa miaka 62 hadi sasa.

Na mke wake amekuwa akiwasiliana nae kwa lugha ya ishara na vitendo, japokuwa bado imekuwa vigumu sana kwa wawili hao kuelewana.

'Imenichukua miaka miwili kujifunza kuwasiliana kwa kutumia mikono, na mara baada ya kufahamu lugha hiyo, alianza kupata matatizo ya kuona. Bado nafikiri hata hilo alikuwa akijifanyisha tu" amesema Dorothy mke wa Barry.

Wanandoa hao walifanikiwa kupata watoto 6 pamoja na wajukuu 13, ambao pia waliaminishwa kuwa Mr.Dawson ana ulemavu wa kusikia.

"Wakati akiwa nyumbani mara zote Mr.Dawson amekuwa akijifaya kiziwi, na siku niliyombamba ni siku ambayo niliona video yake you tube akiwa anaimba kareoke bar usiku, wakati akitakiwa kuwa kwenye kikao kwa ajili ya kutoa msaada, kuanzia hapo nilielewa kila kitu". Amesema Dorothy.

Mwanasheria wa Mr Dawson, Robert Sanchez amekubali kuwa mteja wake amekuwa akiigiza ukiziwi na kuongezea kuwa "Ilikuwa ndio njia pekee ya kuepukana na mke wake ambaye amekuwa akiongea sana".

Robert ameongezea, "Mteja wake hakuwa na maana mbaya ya kutaka kudanganya familia yake ila ndiyo njia pekee iliyofanya ndoa yake idumu kwa kipindi kirefu takribani miaka 62.

"Mteja wangu ni mkimya sana na sio muongeaji, lakini mke wake ni muongeaji na mwenye majibu ya karaha, kama asingedaganya kuwa kiziwi basi ndoa ingekuwa imekwishavunjika miaka 60 iliyopita".

Aidha mwanasheria wake anasema Mr.Dawson alifanya hivyo kwa ajili ya familia yake.

Hata hivyo wawili hao walipandishwa kizimbani, na Dawson amedai kulipwa fidia ya kiasi kikubwa cha pesa kwa mumewe kujifanyisha kuwa na ulemavu huo kwa muda mrefu uliokuwa mzigo kwake.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...