Wednesday, January 27, 2021

Usalama waimarishwa New Delhi baada ya vurugu za wakulima


Polisi nchini India wameweka usalama mkali na kufunga barabara kuu ndani ya mji wa New Delhi, siku moja tu baada ya wakulima kuzusha vurugu katika mji mkuu na kusababisha kifo cha mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Vurugu hizo ziliashiria kilele cha mzozo kati ya serikali na maelfu ya wakulima ambao wamekuwa wakipiga kambi viungani mwa mji huo tangu mwisho wa mwezi Novemba.

Wakulima hao ambao wengi wanatoka majimbo ya kaskazini mwa India likiwemo jimbo la Punjab, wanataka mageuzi mapya katika sekta ya kilimo yafutwe, wakihofia yatawaacha kuhangaika mikononi mwa mashirika makubwa.

Hapo jana wakati wa gwaride la kila mwaka la kitaifa, misafara ya matrekta ya wakulima ilivunja vizuizi vilivyowekwa barabarani kisha wakulima wakaingia katikati ya mji, hatua iliyosababisha makabiliano kati yao na polisi waliotumia marungu na kemikali za kutoa machozi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...