Sunday, January 24, 2021

Urusi yaishutumu Marekani kwa kuingilia mambo yake ya ndani





Urusi imeishutumu Marekani kwa kuingilia mambo yake ya ndani kwa kuchapisha mambo yanayounga mkono maandamano ya kuachiliwa kwa mpinzani wa Urusi Alexei Navalny aliyefungwa gerezani.


Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, ilitangazwa kwamba Ubalozi wa Marekani huko Moscow ulichapisha kwenye mitandao ya kijamii ili kuunga mkono maandamano ya kuachiliwa kwa mpinzani wa Urusi Aleksey Navalnıy.



Katika taarifa hiyo, ambayo imesisitiza kuwa Marekani ilikiuka kanuni za kidiplomasia kwa kuchapisha mambo kama hayo, iliendelea kwa kusema,



"Ubalozi wa Marekani huko Moscow unaingilia mambo ya ndani ya Urusi." 



Vilevile taarifa hiyo imesema kuwa,



"Utawala wa Marekani lazima ushughulikie shida zake yenyewe, kama vile mgawanyiko uliosababishwa na ukosefu wa haki ya kijamii na ukosefu wa usawa katika jamii ya Marekani. Jaribio la kuchochea mambo makubwa ya diplomasia kwa kupuuza kanuni za maadili limekosa kufaulu na litakuwa na athari mbaya kwa uhusiano wa nchi mbili." 



Kupitia mitandao ya kijamii, Ubalozi wa Marekani huko Moscow uliandika saa na maeneo ya maandamano yaliyofanyika jana.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...