Tuesday, January 26, 2021

Taji Liundi "Mama Yetu Alitunywesha Sumu Mimi na Wadogo Zangu, Nipona Wadogo Zangu Wakafariki"

Kwa mara ya kwanza mtangazaji nguli nchini Taji Liundi amefunguka kuhusu maisha yake binafsi na mchango wake katika tasnia ya muziki. Taji Liundi aka Master T ambaye amefanya kazi na vituo mbalimbali vya redio ikiwemo Redio one na Times fm toka miaka ya 1980 amefunguka mengi wakati akihojiwa na kipindi cha Salama Na cha Salama Jabir.


Taji Liundi amesimulia kisa cha kusisimua na kusikitisha ambapo mama yake mzazi aliamua kuwanywesha sumu yeye na wadogo zake watatu tukio lililopelekea wadogo zake watatu kufariki dunia huku yeye (taji) akiponea chupu chupu.


Tukio Hilo lilitokana na mgogoro wa ndoa baina ya mama yao na baba yao kutokana na kukosekana kwa uaminifu hasa upande wa mzee wake, baada ya mama Taji maarufu sana nchini Agnes Doris Liundi kugundua hilo aliazimia kujiua yeye na wanaye na ndiyo kisa cha kuwanywesha sumu wanaye.


Mama Taji alihukumiwa kunyongwa mpaka kufa na Mahakama kabla ya kupewa msamaha wa Rais na Hayati Baba wa Taifa J K Nyerere.


Baba yake Taji Liundi alikuwa mwanasheria, Jaji wa Mahakama Kuu na hatimaye msajili wa vyama vya siasa mwaka 1992.


Pia Taji Liundi ameeleza alivyoanza kutangaza Redio One, kipindi chake alichokianzisha cha DJ Show na kuwa mtangazaji wa kwanza kucheza Bongo Fleva kwenye redio, kabla ya kuwaachia mikoba akina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...