Tuesday, January 19, 2021
Taifa Stars kuanza na Zambia leo michuano ya CHAN
Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Taifa Stars, Mrundi Etienne Ndayiragije amesema "maandalizi yameenda vizuri, wachezaji wapo sawa. Kuhusu korona wamechekiwa wote wako sawa, tuko vizuri. Tunaendeelea kujiandaa kwenye vile ambavyo tunaamini vitakuwa vya msaada kwetu".
Kuhusu nafasi ya Stars kwenye mchezo huo, Ndayiragije amesema " morali na hali ya kujiamini kuko juu kwenye kambi, wachezaji wapo tayari kwa mchezo, nimewaambia tutatcheza ili tushinde maana najua ushindi utainua ari kwenye kikosi na kupelekea tufanye vizuri kwenye michezo inayofuata".
Etienne amesema ari imeongezeka baada ya kocha msaidizi Selemani Matola kujiunga na kikosi hicho baada ya kumaliza majukumu ya kuiongoza kikosi cha Simba kwenye michuano ya Mapinduzi viswani Zanzibar na Erasto Nyoni akijiunga na timu baada ya kumaliza matatizo ya kifamilia.
Ushiriki wa Taifa Stars kwenye michuano ya CHAN umekuja baada ya miaka takribani 11 tokea ushiriki wao mwaka 2009 michuano hiyo ulipoanzishwa na ndiyo msimu ambapo Zambia walishiriki kwa mara ya kwanza na kushika nafasi ya 3 ikiwa ndiyo ya juu zaidi kwa upande wao kwenye CHAN.
Huu utakuwa mchezo wa 18 wawili hao kukutana, kwenye michezo 8 ya mwisho ambayo Stars imekutana na Zambia kwenye michuano tofauti kukiwa na mchanganyiko wa wachezaji wao wakigeni kwenye vikosi vyao, Zambia imeshinda mara 4, sare 3 wakati Stars imeshinda mara 1 pekee.
Ili Taifa Stars iweke hai matumaini ya kufuzu hatua inayofuata ya robo fainali, inahitaji ipate ushindi michezo yote mitatu ya makundi watakayocheza au kuwa na matokeo yatakayomfany awe na alama nyingi kuliko wote kwenye kundi D au alama nyingi zitakazomfanya ashike wapili kwenye kundi.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
