Tuesday, January 19, 2021
Mzee wa Miaka 80 Afia Gesti na Akiwa na Binti
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la David Makerege Mluli (80) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli ya Mbezi Garden iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam akiwa na mpenzi wake aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kibaya (33). Kifo hicho kilitokea muda mfupi tangu wafike hotelini hapo, kwa mujibu wa maelezo ya polisi.
Taarifa ya kifo hicho ilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii juzi na jana, huku ikielezea namna tukio lilivyokuwa kwa wawili hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyokuwa ikizunguka mtandaoni, marehemu ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika katika hoteli hiyo huku akiwa na maji na juisi katika chumba alicholipia.
Neema alipofika inasaidikika kuwa aliagiza chipsi na mishikaki mitatu. Walipokuwa pamoja Neema aliona ghafla mzee huyo akipumua kwa shida ndipo alipokwenda kutoa taarifa mapokezi akiomba msaada.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhan Singai alisema tukio hilo lilitokea Januari 16, 2021 katika hoteli hiyo huku akibainisha kuwa uongozi wa hoteli ndiyo uliopiga simu kuripoti jambo hilo.
"Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa meneja wa hoteli hiyo aitwaye Newton Mkonda kuwa katika chumba namba 22 kuwa kuna mteja amefariki dunia.
"Baada ya taarifa kupokelewa jeshi la polisi lilifika katika eneo la hoteli hiyo na kubaini uwepo wa maiti ya mwanaume ambaye jina lake lilifahamika kupitia kitambulisho kilichokuwapo katika nguo zake," alieleza Kingai.
Alisema mbali na maiti pia katika chumba hicho alikutwa Neema ambaye alijitambulisha kama mpenzi wake marehemu na mkazi wa Goba jijini hapa.
"Katika uchunguzi wa awali uliofanyika, jeshi la polisi lilibaini kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote. Mwili ulichukuliwa na askari waliofika na kupelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kuhifadhiwa," alisema kamanda huyo.
Alisema katika uchunguzi huo pia walibaini kuwa kifo cha marehemu ni cha kawaida kwani licha ya kutokuwa na jeraha ni mkojo pekee ndiyo walibaini ulikuwa umemtoka.
"Bado hatujafikia hitimisho kwani bado tunahitaji kufanya uchunguzi zaidi hasa kupitia kwa madaktari ili kujua kuwa kifo hiki kimetokea kwa sababu gani.
"Tunasubiri ndugu wa marehemu, katika taratibu za uchunguzi lazima kuwe na mtu anatambua mwili huo, sisi tumetambua kwa kupitia vitambulisho na kuoanisha sura yake na iliyopo kwenye vitambulisho, lakini katika uchunguzi wa hospitali hasa ndugu ndiyo wanaopaswa kuthibitisha kuwa huyu ndiyo yule ambaye sisi tunasema amefariki," alieleza.
Kuhusu Neema alisema anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
