Friday, January 8, 2021

SIMBA SC YAACHANA NA KOCHA WAKE MKUU SVEN VAN DENBROECK

 


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck

Na Damian Masyenene
KLABU ya Simba ya Jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2020 imethibitisha kuachana na Kocha wake Mkuu, Mbelgiji Sven Van Denbroeck baada ya kuwa nae kwa misimu miwili na kufanikiwa kutwaa mataji matatu ambayo ni Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho (FA) na Ngao ya Jamii.

Taarifa hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Kocha huyo kuisaidia timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa barani Africa (CCL) baada ya kuichapa timu ya Platinum FC ya Zimbabwe kwa mabao 4 kwa 0 jana katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Soma zaidi taarifa ya Klabu ya Simba hapa chini

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...