Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Masyeba, akizungumza kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Na Marco Maduhu -Shinyanga.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imefanya kikao na watendaji wa Kata kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti katika mwaka wa fedha ujao (2021-2022), ili kubaini vipaumbele muhimu ambavyo vitatekelezeka na kutoa huduma.
Kikao hicho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano katika shule ya Msingi Balina iliyopo Kata ya Ndembezi, na kuhudhuriwa pia na wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema watendaji hao wanapaswa kuainisha vipaumbele vichache na muhimu, ambavyo vitaweza kutekelezeka kuliko kubainisha vitu vingi na kushindwa kutekelezwa kulingana na ufinyu wa bajeti.
"Kipindi hiki ni muhimu sana kwa wananchi cha utoaji wa maoni yao ya mapendekezo ya bajeti ijayo kabla ya kwenda kwenye ngazi za juu, hivyo naomba wananchi watoe mapendekezo yao kupitia kwenye ofisi za watendaji wa kata ili yafanyiwe kazi, kuliko kuanza kulalamika kwenye mitandao ya kijamii,"amesema Mwangulumbi.
Pia amewataka watendaji hao kusimamia kwa ukamilifu zoezi la ukusanyaji mapato, pamoja na wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kulipa kodi na ushuru kwa hiari, ili zipatikane fedha za utekelezaji wa mapendekezo hayo ya bajeti.
Kwa upande wake Mchumi wa manispaa ya Shinyanga Gwakisa Mwasyeba, alisema kikao hicho ni muhumi sana, ambacho kitasaidia kuchambua vipaumbele vya mapendekezo ambavyo ni muhimu vitakavyo zingatia maslahi mapana ya wananchi.
Nao baadhi ya watendaji hao wa Kata akiwamo Rose Matunda kutoka Kitangili na Joshua Masengwa kutoka Kizumbi, wametoa wito kwa wananchi kipindi wanapokuwa wakiitwa kwenye mikutano ya hadhara kutoa maoni ya mapendekezo ya Bajeti, wawe wana hudhulia ili kuondoa malalamiko pale bajeti itakapopitishwa.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kikao hicho cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Masyeba, akizungumza kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Gwakisa Masyeba, akizungumza kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ngazi ya Kata.
Watendaji wa Kata manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha kujadili vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ijayo ngazi ya Kata.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Mwakaluba Wilison, akitoa vipaumbele vya mapendekeo ya Bajeti ijayo kwenye Kata yake.
Ponsian Mgodita Afisa Mtendaji Kata ya Chibe, akitoa vipaumbele vya mapendekezo ya bajeti ijayo kwenye Kata yake.
Gaudiozi Mwombeki, akitoa vipaumbele vya mapendekezo ya Bajeti ijayo kwenye Kata yake.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.