Msanii Harmonize ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya Konde Gang Music Worldwide, amekoshwa na ngoma tatu za Ibraah ambazo amezitoa kwa pamoja na kuzipata jina la Karata 3.
Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram, amehoji kwa Ibraah juu ya maneno yaliyopo kwenye ngoma iitwayo Mepenzi.
''Mdogo angu Ibraah unajua uzito wa haya maneno...?? au umejiimbia tuu..!!!! daaaah dunia hiii sawa bana'', - sehemu ya maneno ya Harmonize.
Kwa upande wake Ibraah yeye amejibu, ''Kakaangu mimi nafikisha ujumbe tu ila sijuwi huwenda ninge kuwa nayajuwa nisinge imba kabisa. Pole sana kaka ila huu wimbo umewagusa watu wengi sana hakika mungu Aniepushe na haya lio wakuta wa kubwa zangu #NIMPENDE nae Anipende Aposawa''.
Pia Harmonize amesifia ngoma ya nyingine kwenye Karata 3 iitwayo Upande ambayo Ibraah amefanya collabo na Young Skales kutokana Nigeria.
''This one is so special 2 me to see my (2) brother's in one record been dreaming this'', ameandika Harmonize.
Source