Inaarifiwa basi hilo lilikuwa likitoka upande wa Pwani Kusini kuelekea Mombasa wakati kisa hicho kilifanyika kwenye kivukio cha Likoni.
Walioshuhudia kisa hicho wanasema dereva wa basi hilo alipoteza mwelekeo alipokuwa akijaribu kuingia kwenye feri.
Ni dereva na utingo wake waliokuwa kwenye basi hilo na walishauriwa kuruka nje huku basi likiendelea kuzama.
Video kwenye mitandao zilionyesha wakazi wamejawa na hofu huku wakishauri waliokuwa ndani kuruka nje. Wawili hao waliruka na kuokolewa na mashua iliyokuwa ikipiga doria baharini.
Aidha maafisa wa shirika la feri pia wamefaulu kuiokoa basi hiyo isizame.
Mtandao wa Nation , umeandika kuwa basi liliteleza kutoka kwenye feri na kuingia ndani ya majira ya saa nne asubuhi ,hatua chache kabla ya eneo la nchi kavu.
Dereva na kondakta wameokolewa wote na polisi pamoja na walinzi wa kivuko.
Basi hilo la Yutong luxury lilikuwa linatokea Diani where ambapo lilikuwa limewapeleka watalii waliowasili Mombasa hapo jana.
Ingawa kuna basi lingine kutoka kampuni hiyo hiyo lilifanikiwa kuingia kwenye feri likiwa salama.
Dereva wa basi hilo bwana Salim Omar amewaambia polisi kuwa alishindwa kulidhibiti gari kuanguka majini baada kunaza kuteleza, na kulikuwa na mvua iliyonyesha majira ya asubuhi.
"Nilikuwa karibu nafika feri lakini basi likanizidi nguvu na kuanguka,Ninamshukuru tu Mungu kuwa tuko salama," alisema bwana Omar, ambaye alikuwa bado anatetemeka.
Alisema amekuwa akivuka likoni wakati anaendesha kwa miaka 11 na hajawahi kukutana na tukio la namna hii, hii ni mara ya kwanza.