Friday, January 1, 2021

Breaking : BENARD MEMBE AIPIGA CHINI ACT WAZALENDO


Aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo na mshauri wa Chama hicho, Bernad Membe leo Januari 1,2021 ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama hicho.

Membe ametangaza uamuzi huo akiwa nyumbani kwake kijijini Rondo Chiponda, Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi ambapo amesema hajafanya uamuzi huo kwa shinikizo lolote na kwamba kwa sasa atakuwa mshauri wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi ya Tanzania na kupigania demokrasia ya kweli.

Benard Membe alitangaza kuhamia  Chama cha ACT Wazalendo siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 akitokea Chama Cha Mapinduzi kisha kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho ingawa hata hivyo kuliibuka migogoro ndani ya chama hicho hadi kufikia hatua ya kutambua nafasi yake hiyo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...