Wednesday, January 27, 2021

Biden aanza na rais wa Urusi: Putin usituingilie hayakuhusu



Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi katika mawasiliano yao ya kwanza kwa njia ya simu, White House imeeleza.



Mazungumzo hayo ni pamoja na majadiliano kuhusu maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini Urusi na kuongezwa kwa mkataba wa silaha za nyuklia wa Marekani na Urusi

Bwana Putin alimpongeza rais mpya wa Marekani kwa kushinda uchaguzi,kwa mujibu wa taarifa ya Urusi.

Pande zote mbili zilisema zilikubaliana kudumisha mahusiano.

White House na Kremlin zimesema nini kuhusu mazungumzo yao?

"Rais Biden aliweka wazi kuwa Marekani itasimama kidete kutetea maslahi ya taifa lake kwa vitendo vya Urusi vinavyotuathiri sisi au washirikawetu," ilisema taarifa ya Marekani.

Ikulu ya Marekani imesema marais hao waliozungumza kwa simu siku ya Jumanne pia walijadili kuhusu mashambulizi ya mtandaoni ya kampuni ya SolarWinds, ambayo kwayo Moscow ilinyooshewa kidole, ripoti zikieleza kuwa Kremlin iliwafadhili wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, na sumu ya mwanaharakati wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny.

Maafisa wa urusi wamesema Bw. Putin "ameona kuwa kuweka sawa mahusiano kati ya Urusi na Marekani kutafanya kufikiwa kwa malengo na kulinda maslahi ya nchi zote mbili-ukizingatia jukumu walilonalo la kulinda usalama na uimara duniani.

"Kwa ujumla, mazungumzo kati ya viongozi wa Urusi na Marekani yalikuwa ya biashara na ya asili ya kweli," taarifa ya Kremlin iliongeza.

Viongozi hao wawili walionekana kutia saini makubaliano ya kurejesha New Start, makubaliano ya wakati wa Obama ambayo yanapunguza viwango vya silaha, makombora na virusha makombora miongoni mwa silaha za nyuklia za Marekani na Urusi.

Ulipaswa kumalizika mwezi ujao, na Bw Trump alikuwa amekataa kusaini.

Biden
Biden hatafuti makabiliano
Joe Biden alikuwa ameonesha atakuwa mkali kwa Vladimir Putin kuliko Donald Trump, ambapo mara nyingi alitia shaka kuhusu kuingilia kwa Urusi katika uchaguzi wa 2016.

Bwana Biden anaripotiwa kuwa alimwambia Putin kwamba anajua Urusi ilijaribu kuingilia kati uchaguzi wa 2016 na 2020. Pia alimuonya rais wa Urusi kwamba Marekani ilikuwa tayari kujitetea dhidi ya ujasusi wa kimtandao, na mashambulio mengine yoyote.

Licha ya njia ya maridhiano ya Bwana Trump, Kremlin haikufaidika na urais wake, kwa sababu utawala wake uliwawekea vikwazo sana Warusi kwa masuala kutoka Ukraine hadi kushambulia wapinzani. Joe Biden na timu yake ya sera za kigeni watachukua msimamo thabiti kuhusu haki za binadamu na nia ya Bwana Putin huko Ulaya.

Lakini hawatafuti makabiliano.

Badala yake, wanatarajia kusimamia uhusiano na kushirikiana pale inapowezekana. Hivyo basi marais hao wawili walikubaliana kufanya kazi kumaliza kukamilisha mkataba mpya wa kudhibiti silaha kabla ya kumalizika mwezi ujao.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...