Tabia za ujasiriamali zinaweza kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na kuzifuata,lakini tabia zingine hazifundishiki hizi ni zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti katika kufikili,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo ambazo haziwezi kufundishika.
Jambo la kutia moyo ni kwamba tabia ambazo zinafundishika ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika biashara.
Zifuatazo ni tabia za ujasiriamali;
Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo, anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelevu wa kutambua mabadiriko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
Kuwa na uwezo wa kuongoza
Mjasiriamalia lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai uongozi ni kalama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu, ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza, lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiliamali uongozi ni jambo muhimu sana, mjasiliamli lazima aweze kuogoza biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinu za uogozi ili apate matunda kwa Kile ambacho anafanya.
Kuthubutu
Hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa hasara, hawajui jinsi ya kuendesha mradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni lazima awe na uwezo wa kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha il baadaye limletee tija. Waswahili mwanasema "uwoga ni umaskini".
Nidhamu
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, mjasiriamali lazima awe na nidhamu katika biashara yake,awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kakazi kwa bidii. Nidhamu ni hanzo ch mafanikio. Mfano mfanyabiashara wa duka ni lazima uwe na nidhamu kwa wateja wake ili wasimkimbie.
Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu kikubwa hapa ni lazima mjasiriamli awe anaipenda kwa dhati shughuri anayofanya hii itamasahidia kufanya kazi kwa moyo. Kama unapenda kazi unayo fanya basi kazi HIyo haitakuwa Ngumu bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwako ni hobi na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na maarifa, hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii ili uweze kufanikiwa zaidi kwa kile ukifanyacho.
Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo katika kila jambo alifanyalo, wateja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkweli. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uamifu na ukweli ili upate wateja wengi,lazima uwe mkweli katika bei zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako.
Dhamira
Mtu yeyote anaweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha, kufanya kazi kwa didii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhaira. Lengo au dhamila ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au mradi fulani.
Kwenda na wakati
Mjasiriamali lazima aende na wakati iliaweze kutambua mabadiriko mbalimbali yanayo jitokeza katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa nafasi mjasiriamaili kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko huria, kwenda na wakati pia kunatoa fulsa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na kusoma magazeti, kufanya utafiti.
Tabia ambazao zimeorodheswa hapo juu ni tabia za ujumla ambazo mjasiriamali anatakiwa kuwa nazo,lakini kama huna baadhi ya tabia hizo usifadhaike kwani ujasiriamalia ni somo na sio kipaji
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
