Sunday, December 6, 2020

Picha : MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA MTANGAZAJI WA REDIO FARAJA JENIPHER MAHESA

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Jenipher Mahesa

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamia ya wakazi wa Shinyanga na maeneo jirani wamejitokeza kwenye Mazishi ya Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Redio Faraja Fm Stereo Jenipher Mahesa (32) aliyefariki dunia siku ya Ijumaa Disemba 4,2020 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Jenipher Mahesa amefariki dunia wakati akipata matibabu baada ya kupata ugonjwa wa kupooza tangu tarehe 5.7.2020 na kutibiwa katika hospitali mbalimbali lakini hali yake ilibadilika zaidi tarehe 23.11.2020 na kupelekea kifo chake tarehe 4.12.2020.

Mazishi ya marehemu Jenipher Mahesa yamefanyika leo Jumamosi Disemba 5,2020 jioni katika makaburi ya Dodoma yaliyopo kata ya Ndembezi Mjini Shinyanga.

Akitoa salamu za rambirambi, Mkurugenzi wa Redio Faraja Padre Anatoly Salawa amesema Redio Faraja na Kanisa Katoliki limepoteza mfanyakazi mchapakazi aliyeipenda sana kazi yake akieleza kuwa Jenipher alikuwa Mwandishi Mahiri wa Habari na aliyebobea katika vipindi vya dini.

"Jenipher Mahesa alikuwa mfanyakazi mchapakazi sana. Anatambulika kwa umahiri wake mkubwa katika habari na utangazaji wa vipindi vya dini. Tumeondokewa na nguvu kazi kubwa, Jenipher aliipenda sana Radio Faraja",amesema Padre Salawa.

"Kupitia kazi yake kama mwanahabari amewaelimisha wana Shinyanga, amewaburudisha kupitia kazi yake  ya uandishi wa habari, amekuwa mpishi mzuri wa habari, mchango wake ni mkubwa sana kama mwanahabari. Msiba huu siyo wa Radio Faraja tu bali ni kwa watu wote wanaomfahamu na wanaotambua kazi zake",ameongeza Padre Salawa.

Naye Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari (Shinyanga Press Club – SPC) , Kosta Kasisi amesema Jenipher alikuwa mwanachama wa SPC wa pekee sana kutokana na upole, upendo, nidhamu na unyenyekevu kwa waandishi wa habari wenzake na wadau wa habari.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi, Solomon Nalinga Najulwa amesema Jenipher Mahesa alikuwa ni mtu aliyejitoa sana katika masuala ya kijamii na alikuwa mstari wa mbele kupigania masuala ya haki za watoto na wanawake.

Jenipher Paul Mahesa alizaliwa tarehe 23.3.1988 amefariki dunia tarehe 4.12.2020, ameacha watoto wawili wadogo wa kike.


Jenipher Mahesa enzi za uhai wake
Gari lililobeba mwili wa marehemu Jenipher Mahesa likiwasili nyumbani kwake mtaa wa Dome Ndembezi Mjini Shinyanga kutoka hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Disemba 5,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msafara wa magari yakifuatana na mwili wa marehemu

Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Jenipher Mahesa
Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Jenipher Mahesa
Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Jenipher Mahesa
Ibada ya mazishi ikiendelea
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Nalinga Najulwa akitoa salamu za rambirambi
Mhariri Mkuu wa Redio Faraja, Simeo Makoba akitoa salamu za rambirambi
Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Kosta Kasisi akitoa salamu za rambirambi
Mwandishi wa habari wa Redio Faraja, Moshi Ndugulile akisoma historia fupi ya marehemu Jenipher Mahesa
Mkurugenzi wa Radio Faraja , Padre Anatoly Salawa akitoa salamu za rambirambi
Waandishi wa habari wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenipher Mahesa
Mazishi yanaendelea

Ndugu/familia ya Jenipher Mahesa wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kaburi la marehemu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...