Tuesday, December 29, 2020
MAMIA WAMUAGA MNGEREZA DAR ES SALAAM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema Taifa limepata pigo kwa kuondokewa na Mtendaji wake mchapakazi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza.
Waziri Bashungwa ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Mngereza katika viwanja vya Karimjee.
Amesema katika uhai wake Mngereza alisimamia Tasnia ya Sanaa na kuleta mabadiliko miongoni mwa Wasanii ambao wengi wao walifanya kazi zao kwa kuzingatia mila na desturi za Mtanzania.
Kwa mujibu wa Waziri Bashungwa, Serikali itaendeleza mambo mazuri aliyoyaacha Marehemu Mngereza, yaliyokuwa na lengo la kuleta mabadiliko kwa Wasanii na kazi zao.
Awali akimkaribisha Waziri Bashungwa, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbasi amewataka Wasanii nchini na Watanzania wote kumuenzi kwa vitendo Marehemu Mngereza aliyejitolea na kuipenda kazi yake hadi umauti unamkuta.
Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria shughuli hiyo ya kumuaga Marehemu Mngereza katika viwanja vya Karimjee ni Naibu Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge.
Mwili wa Mngereza unasafirishwa mchana huu kuelekea Suji, Same mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya.mazishi yatakayofanyika kesho.
Mngereza ameacha Mke na Watoto Watatu, ,Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...