Kila siku huwa tunapenda kuwaambia wanawake ni warembo. Neno hili limewaingia katika akili zao kiasi cha kuwa ile maana msingi ya neno 'wewe ni mrembo' imepotea. Hii ni kwa sababu baadhi ya wanaume wasiojua kutongoza wanaishia kulitumia neno hili vibaya kiasi cha kuwa neno hili limepoteza uhalisia.
Je ulikuwa wajua kuwa wanawake hupenda kusifiwa? Na ulikuwa ukijua kuwa kumsifia mwanamke mara kwa mara ni njia moja wapo ya kutongoza? leo tumekuja na mambo tofauti ambayo unapaswa kutumia ili umshawishi mwanamke kuwa ni mrembo, na wala hataona kama ni maneno unalompakizia ama maneno ambayo ameyazoea kuyaskiliza awali.
Twende pamoja:
Jambo la kwanza
Wakati unapotaka kumsifia mwanamke kuwa ni mrembo, usimwambia, "Wewe ni mrembo" mara kwa mara kwa sababu itafikia mahali flani neno hilo litaisha ladha. Badala yake tafuta sehemu muhimu kutoka kwa mwili wake ambayo utaitumia kama kigezo cha kumsifia. Kwa mfano kama umependezwa na pua yake mwambia, "Nimependezwa na pua yako, kila mara nikiiona najiskia na furaha." Ama kama umependezwa na mashavu yake unaweza kumwambia, "Mashavu yako ndio nuru ya macho yangu, yanapendeza." Kumwambia mwanamke maneno kama haya yatamfanya atamani kuwa kando yako. Pia ataona kuwa unamwona anapendeza, unamakinika kuuona urembo wake kupitia kwa viungo vyake vya mwili.
Jambo la pili
Kumsifia mwanamke urembo wake hakuhusishi ngozi yake ya nje pekee, bali pia sehemu yake ya ndani, yaani nafsi yake. Wanaume wengi huwa wanamakinika kumsifia mwanamke umbo, sura na shepu yake huku wakisahau kuwa nafsi ya mwanamke ina umuhimu. Kumsifia mwanamke kwa ujasiri wake, ubunifu wake, hekma, na ujanja kutakupa mkono wa mbele zaidi wakati unapomtongoza ama unapomshawishi. Jambo hili tulishawahi kulizungumzia katika moja ya hatua ya kumtongoza mwanamke ambaye hayuko ligi sawa na wewe. Kumshawishi na kumsifia mwanamke nafsi yake kutamfanya ajiunganishe na wewe zaidi kuliko mwanamke yeyote yule, hivyo hatua iko kwako sasa.
Jambo la tatu.
Unapomsifia mwanamke usitumie maneno hayo kwa hayo. Yaani wewe kila siku ukikutana na yeye unamwambia, "Nakupenda, leo umeangaza nafsi yangu." Matumizi ya neno moja siku nenda siku rudi kutamfanya mwanamke atilie shaka iwapo unasema maneno hayo ndani ya moyo wako ama unasema kumridhisha tu. Well, mbona usije na misamiati mipya? Ama mbona usije na maneno ambayo angetamani kuyaskia? Ukitumia maneno kama 'hurulaini', 'malkia, leo nimekuja kwa milki yako', 'ua langu la waridi' nk kutamfanya mwanamke akupende zaidi na zaidi. So anza kutafuta maneno ambayo anayapenda. Usiingiwe na uvivu wa kutumia maneno hayo kwa hayo kila siku. Kumbuka hapa unataka kuwa bora zaidi kati ya wanaume wale wengine. Chukua hatua sasa.
Jambo la nne
Wakati ambapo umeamua kumsifia mwanamke kama huyu, hakikisha kuwa unamwangalia machoni. Kama ni mwanamke ambaye ndio unaanza kumfukuzia basi jenga confidence ya kumwangalia machoni. Usimsifie huku ukiangalia pembeni ama kuangalia kando. Kumbuka wewe ni Mwanaume Alpha, na wanaume alpha huwa hawatatiziki kama wanatoa hisia zao kuhusu wanawake wanaowapenda.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
