Saturday, December 12, 2020

Diwani wa CUF aipigia debe ilani ya CCM

 


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Diwani kata ya Milola, manispaa ya Lindi anayetokanana Chama Cha Wananchi- CUF ( CUF), Hussein Kimbyoko ameahidi kutekeleza kikamilifu ila ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) katika kipindi chake cha uongozi.


Mheshimiwa Kimbyoko alitoa aahadi hiyo jana baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa nafasi ya meya na makamo meya wa halmashauri ya manispaa ya Lindi. Ambapo yeye alikuwa mgombea wa kiti cha meya wa halmashauri hiyo.


Kimbyoko alisema licha ya kushindwa kuchaguliwa lakini atatekeleza illani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2525. Kwani ni ilani ya chama kilichounda serikali. Kwahiyo katika kipindi chake uongozi ataongoza kwakutumia yaliyomo kwenye ilani hiyo.


Diwani huyo pekee wa CUF katika baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Lindi lenye madiwani 44 wakiwamo wabunge wa wawili wa majimbo ya Mchinga na Lindi mjini alisema licha ya kuangushwa na mgombea wa CCM, Frank Magali ambae ndiye meya wa halmashauri hiyo lakini atampa ushirikiano. Kwani wote watatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.


Kimbyoko alikwenda mbali kwakusema aligombea nafasi hiyo wakati anajua asingeshinda. Lakini kwakuwa yeye siyo muwoga na haogopi mapambano aliamua kugombea.


" Mwanajeshi hajisikii fahari kufia nyumbani na kuogopa vita. Bali hujisikia fahari kufia vitani kwa heshima. Nilijua nitakufa, lakini nimekufa kwaheshima kwenye uwanja wa mapambano nikiwa jeshi la mtu mmoja," alisema Kimbyoko.


Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi, Abdallah Madebe licha ya kumshukuru na kumpongeza alimuomba ashirikiane nae katika ushauri wa jinsi ya kutekeleza ilani ya CCM. Kwani yeye ndio kiongozi wa chama chenye ilani aliyoahidi kutekeleza.


Kwenye nafasi ya Umeya wa halmashauri ya manispaa ya Lindi, diwani wa kata ya Kitumbikwela, Frank Magali wa CCM alishinda. Nibaada ya kupata kura 41 kati ya 43 zilizopigwa. Wakati Kimbyoko akipata kura mbili.


Aidha diwani wa kata ya Nangaru, Salum Ng'ondo ambaye hakuwa na mshindani alichaguliwa kuwa makomo meya. Nibaada ya kupata kura 42 za ndio kati ya 43 zilizopigwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...