Monday, November 16, 2020
Timu ya wasichana U-17 yarejea nchi na ubingwa COSAFA
Kikosi cha timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17 'Tanzanite Queens' kimetua hapa nchini usiku wa kuamkia leo wakitokea nchini Afrika Kusini ambapo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Tanzania ilitwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga Zambia kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela Bay baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo, Zambia walikuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa dakika ya 19 na mshambuliaji Comfort Seleman ambaye alitumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Tanzania baada ya kuondoka na mpira kuanzia katikati ya uwanja hadi kwenye goli na kupiga shuti ambalo lilimsinda golikipa Aisha Mrisho.
Lakini kipindi cha pili Tanzania ilisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Koku Kipanga baada ya Aisha Masaka kuchezewa madhambi ndani ya eneo la 18 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Akizungumza mara baada ya kuipokea timu hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallece Karia amesema kuwa, wakati timu hiyo inaondoka aliwataka wachezaji hao pamoja na wale wa timu ya wakubwa, Twiga Stars kuhakikisha mmoja wao wanarudi na kombe hilo ikiwa kama zawadi kwa viongozi wapya wa serikali waliopata ushindi wa kishindo.
Amesema, anafurahi kwa kuwa timu hiyo imekuwa ya kwanza kutoa zawadi ya ushindi kwa viongozi hao na jambo kubwa kwa sasa ni kuomba kupata sapoti kwaa ajili ya vijana hao wa kike na kiume kwani ndio msingi wa timu nzuri za Taifa kwa miaka ijayo.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
