Monday, November 9, 2020

Saudi Arabia hatimaye yampongeza Joe Biden kwa ushindi wake


Hatimaye Saudi Arabia imempongeza Joe Biden jana kwa ushindi wake wa uchaguzi wa Marekani baada ya kumshinda Donald Trump ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu wa kibinafsi na mwanamfalme Mohammed bin Salman. 

Wakati ambapo mataifa mengine ya Kiarabu yalikuwa yanatoa pongezi kwa Biden ambaye amechaguliwa kwa tiketi ya chama cha Democratic Mohammed bin Salman alikuwa kimya kuhusiana na suala hilo licha ya kuwa alitoa pongezi kwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwa muhula wa pili. 

Biden ambaye ni makamu wa rais wa zamani wa Marekani wakati wa kampeni aliapa kuangazia upya mahusiano ya Marekani na Saudi Arabia akisema atahitaji uwajibikaji kutoka kwa ufalme huo kuhusiana na kifo cha mwandishi wa habari Jamal Khashoggi aliyeuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia huko mjini Istanbul-Uturuki, na pia Marekani itasita kuunga mkono vita vya Yemen.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...