Familia ya milionea maarufu nchini Zimbabwe, Ginimbi Genius Kadungure - aliyefariki na ajali ya gari Novemba 8, inasema watu watakaoudhuria mazishi ya milionea huyo siku ya Jumamosi lazima wavaa nguo nyeupe.
Mavazi hayo meupe yatavaliwa kama sawa na wakati alipokuwa hai, aliandaa sherehe na kutaka kila mmoja apendeze kwa kuvaa nguo nyeupe.
Vilevile alikuwa anawakumbusha mara nyingi kuwa hivyo ndivyo angependa kuzikwa , watu wasiwe na haraka haraka ya kumzika na wavae nguo nyeupe katika mazishi yake.
"Mchukue muda kupanga mazishi yangu. Nitahitaji kila anayehudhuria mazishi yangu avae nguo nyeupe tu, kupendeza ni lazima siku hiyo.
Tafadhali kumbuka kuchukua muda wenu muwezavyo kupanga mazishi yangu. Kumbuka ,nitakuwa nimevalia nyeupe tu. Hicho tu ndio ninakihitaji kwenye mazishi yangu." Juliet ambaye ni dada yake alinukuu maneno ya kaka yake alivyosisitiza kabla ya kifo chake.
Ginimbi Genius Kadungure, alifariki siku ya Jumapili , majira ya asubuhi katika mji wa Borrowdale, Harare, Zimbabwe.
Jina lake halisi ni Genius Kadungure na alikuwa maarufu kwa jina la Ginimbi.
Aizaliwa Oktoba 10,mwaka 1984. Hivyo amefariki akiwa na miaka 36.
Alikuwa mfanyabiashara maarufu , alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya Piko Trading Holdings & Founder of Genius Foundation, na mmiliki wa klabu ya Sankayi (AKA Dreams Nightlife Club).
Alikuwa na 'Master of Business Administration - alipata MBA yake katika chuo kikuu cha at Great Zimbabwe.
Aliishi: Govan Mbeki, Mpumalanga, Afrika Kusini ingawa nyumbani ni Harare, Zimbabwe.

