Rais mteule wa Marekani Joe Biden amemchagua mshauri wake wa zamani Ron Klain kama Mkuu wa wake wa utumishi.
Katika taarifa aliyoitoa usiku wa kuamkia leo Biden amesema amemchagua Klain kuchukua nafasi hiyo kwa kuwa uzoefu wake wa muda mrefu utamsaidia kukabiliana na changamoto zitakazotokana na kazi hiyo.
Klain ataongoza shughuli za ikulu ya White House ambayo bila shaka itakuwa imejikita katika kukabiliana na janga la virusi vya corona linaloendelea kuenea kote nchini humo.
Atakabiliwa pia na changamoto ya kufanya kazi na bunge la Congress lililogawika ambalo huenda likajumuisha bunge la seneti linaloongozwa na Warepublican.
Klain pia alihudumu kama mratibu wa kukabiliana na janga la Ebola mwaka 2014.
