Friday, September 18, 2020

RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA BARABARA YA TEGETA NYUKI KUKAMILISHA UJEZI IFIKAPO MWEZI OKTOBA, "AKIKAIDI PATACHIMBIKA"


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge
Na Azmala Said - Dar es salaam 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge ametoa mwezi mmoja kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa barabaara ya Tegeta Nyuki yenye urefu wa Kilometa 1.06 kuhakikisha anakamilisha kwa wakati  na kueleza kuwa endapo atashindwa kutekeleza agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

RC Kunenge ametoa maagizo hayo wakati Wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amesema mkandarasi huyo wa Kampuni ya CMG Construction amekuwa akisuasua kumaliza mradi licha ya kuongezewa muda ambapo amewaelekeza TARURA kumsimamia ipasavyo Mkandarasi huyo.

Aidha RC Kunenge pia ametembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Stand Mpya ya kisasa Mbezi Louis ambayo ujenzi wake umefika 80% na inagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 56 ambapo ameonyesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi ilipofikia.

Akiwa kwenye ukaguzi wa Barabara ya Madale - Wazo yenye urefu wa Km 6 inayogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 9.9, Kunenge amefurahishwa na juhudi za mkandarasi huyo huku akieleza kuwa barabara hiyo ikikamilika itakuwa "shortcut" nzuri ya kutoka Mbezi kupitia Madale hadi Wazo.

Katika ziara hiyo Kunenge pia ametembelea ujenzi wa Daraja la Ulongoni A lililopo Kata ya Gongolamboto ambalo ujenzi wake unagharimu Shilingi Bilioni 4.3 na Ujenzi wa Daraja la Ulongoni B ambapo amewahimiza wakandarasi kuongeza juhudi ili ujenzi ukamilike ndani ya Muda uliopangwa ili kupunguza kero walizokuwa wakizipata wananchi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...