Waziri mkuu wa Lebanon Hasan Diab alitangaza kujiuzulu kufuatia mlipuko huo ambao umesababisha maafa makubwa nchini Lebanon.
Wito huo umetolewa na Ufaransa muda mchache baada ya waziri Hasan Diab kutangaza kujiuzulu kwake katika wadhifa wake wa waziri mkuu wa Lebanon.
Kwa mujibu wa Ufaransa , hali iliopo nchini Lebanon inastahili inatakiwa kupatia ufumbuzi kwa ajili ya kukidhid matkwa ya raia ambao wanahitaji kusikilizwa na kuhudumiwa katika kipindi hiki kigumu.
Rais wa Ufaransa alifanya ziara nchini Lebanon baada ya janga mablo limekumba taifa hilo.
Viongozi tofauti akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Uturuki walikwenda nchini na baade kufuatia msaada wa vifaa vya matibabu na madaktari ambao wanawahudumia majeruhiwa wa mlipuko uliotokea mjini Beyruth.