Saturday, July 11, 2020
Polisi yafanikiwa Kumkamata Dereva Aliyesababisha Ajari ya Watu 10 Mlima Kitonga
JESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Iringa limefanikiwa kumkamata dereva wa basi la Prezdar Said Abas Said (30) aliyesababisha ajali eneo la mlima Kitonga iliyopelekea vifo vya watu 10 na majeruhi 36.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwire alisema kuwa mara baada ya ajali hiyo dereva huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kujificha kwa baba yake mdogo maeneo ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Alisema kuwa Juni 27 katika mlima Kitonga wilaya ya Kilolo kulitokea ajali ya basi lenye namba za usajili T 326 CSX aina ya Yutong linalojulikana kwa jina la kibiashara Prezdar likifanya safari zake Iringa kwenda Dar na kusababisha vifo vya watu 10 na kujeruhi watu 36.
Kamanda Bwire alisema kuwa basi hilo liliacha njia kwenye mlima Kitonga na kutumbukia bondeni ambapo dereva wa basi alikimbia mara baada ya ajali hiyo na jeshi la polisi kumtaka mmiliki wake Neechi Msuya kuwapa ushirikiano wa kumpata dereva huyo.
Alisema kuwa mmiliki wa basi hilo, Neechi Msuya (40) mkazi wa Dar es Salaam alijisalimisha kituoni Juni 30 mwaka huu ambapo jeshi la polisi liliendelea na msako wa kumtafuta dereva huyo hadi kumpata akiwa amejificha wilaya ya Mbarali.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na upelelezi na pindi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria za usalama barabarani.
Naye Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Yusuph Kamota amewataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani hasa wanapokuwa katika katika mkoa wa Iringa na kuomba msaada kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kupata maelekezo pindi wakiona hawaelewi kuhusu mlima Kitonga.
Alisema kuwa madereva wanatakiwa kutii sheria bila shuruti na endapo ikitokea ajali wajisalimishe kwa kifungu cha sheria za usalama barabarani namba 57 hata kama dereva alikuwa amechanganyikiwa kiasi gani anapewa masaa 12 kuweza kujisalimisha.
Alisema kuwa mtu yoyote ambaye ni dereva asipojisalimisha ndani ya masaa kumi na mbili atakamatwa tu kwani jeshi lina mkono mrefu na macho makali kuweza kubaini wanaokimbia kama ambavyo wameweza kumkamata dereva wa basi la Prezdar.
Kamota alisema kuwa kwa upande wa kikosi cha usalama barabarani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu ambayo imepunguza matukio ya ajali mkoani hapa na kufanya doria za barabarani usiku na mchana kwa lengo la kukabiliana na ajali.
Alisema kuwa vyanzo vya ajali viko vingi lakini makosa ya ajali yanasababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia asilimia 76 ya ajali hivyo vyanzo kama mwendo kasi, ulevi, kutofata sheria za usalama barabarani kwa ujumla vinadhibitiwa na jeshi hilo kwa njia ya doria.
'' Sisi kama jeshi tumejipanga vyema kabisa natoa wito kwa madereva wawe na tahadhari katika maeneo hatarishi kama mlima kitonga na bora uwe makini kuuliza kuliko kwenda kusababisha ajali ambazo zinasababishwa na madereva wazembe'
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
