Saturday, May 2, 2020
Undani wa Kisa cha Mwanamke Aliyewapikia Mawe Watoto Wake na Muujiza Uliotokea
Kipande cha video kilichotua mtandaoni kikimuonesha mwanamke mjane raia wa Kenya akiwapikia mawe wanaye wanane kwa lengo la kuwadanganya kuwa anawapikia chakula ili walale na kuvusha usiku, kimebadili maisha ya mwanamke huyo baada ya kupokea mamilioni ya fedha kutoka kwa 'Wasamalia wema'.
Peninah Bahati Kitsao, mwanamke mjande anayeishi Mombasa nchini Kenya alirekodiwa na jirani yake, Prisca Momanyi katika harakati za kuwadanganya watoto wake baada ya kukosa chakula cha kuwapikia. Aligusa mioyo ya watu wengi hasa baada ya kuhojiwa na kituo cha runinga cha NTV.
Bi. Manyoni ndiye aliyekifikisha kipande cha video hiyo mtandaoni na kuvifikishia taarifa vyombo vya habari ili kujionea uhalisia wa ugumu wa maisha uliokuwa unamkabili jirani yake.
Katika mahojiano aliyofanya na NTV, Bi. Kitsao mwenye watoto nane, asiyejua kusoma na kuandika, alieleza kuwa alikuwa anafanya kazi za kuwafulia nguo watu majumbani kwao, lakini hivi sasa hali imekuwa ngumu baada ya mwingiliano wa watu kuzuiwa kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona.
Mwanamke huyo mwenye watoto nane anaishi kwenye nyumba duni yenye vitanda viwili vya kulala. Mume wake alipoteza maisha mwaka jana baada ya kuvamiwa na majambazi waliomuua kwa vipigo.
Kupitia mahojiano hayo, alisema kuwa wanae nane walibaini kuwa alikuwa anawadanganya kwa kwakuwa alipika kwa muda mrefu 'mawe yake', lakini hakuwa na jinsi.
"Wanangu walianza kuniambia kuwa wanajua nawadanganya, lakini sikuwa na jinsi kwakuwa sikuwa na kitu chochote," Bi. Kitsao alisimulia.
Jirani yake alilazimika kufika kwenye nyumba hiyo baada ya kusikia watoto wakilia sana usiku huo. Ndipo alipokutana na mbinu ya 'kupika mawe' iliyomuumiza moyo.
Baada ya habari yake kuwa maarufu mitandaoni, jirani yake alipewa mamlaka ya kukusanya michango kupitia akaunti ya benki na simu benki; ndipo makampuni na taasisi yalipomuunga mkono ikiwa ni pamoja na 'Shirika la Msalaba Mwekundu'.
Serikali ya Kenya imeandaa mpango wa kugawa vyakula kwa watu wasiojiweza katika maeneo ambayo watu wamezuiliwa majumbani kwao (lockdown). Kwa habati mbaya mpango huo ulikuwa bado haujapiga hodi kwa Bi. Kitsao. Hadi sasa nchi hiyo ina visa 395 vya corona na vifo 27 vilivyotokana na ugonjwa huo.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
