Friday, May 1, 2020

Shilingi 1.9 bilioni hazijalipwa kwa wakulima katika chama cha RUNALI



Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wakati baadhi ya wakulima wa korosho wakilalamika kutolipwa  malipo ya msimu wa 2019/2020. Imeelezwa kwamba shilingi 1,900,197,234.00 hazijalipwa kwa wakulima waliopeleka korosho zao katika chama cha ushirika RUNALI.

Akisoma taarifa fupi ya ununuzi wa korosho msimu wa 2019/2020 wakati wa kikao cha tathimini ya ununuzi wa zao hilo kwa msimu huo na maandalizi ya ununuzi wa ufuta katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Lindi idara ya kilimo na uchumi, Majdi Myao alisema kiasi hicho cha fedha hakijalipwa na wakulima wanaendelea kudai.

Myao alisema  kampuni  zilizonunua korosho katika mnada wa 13 na 14 hazijalipa kiasi hicho cha fedha kwa RUNALI.

Hivyo kusababisha baadhi ya wakulima waliopeleka korosho zao katika chama kikuu hicho kushindwa kulipwa hadi sasa.

Myao alizitaja kampuni hizo kuwa ni  3B&D Holding Co, Ltd inayodaiwa shilingi 1,073,456,423.00 na Jaharin Commodities Ltd ambayo nayo inadaiwa shilingi 826, 740,811.00.

'' Kampuni ya 3B&D Holdings Ltd hivi karibuni imeendelea kupunguza kiasi cha fedha ambacho inadaiwa imelipa shilingi 150,000,000.00 na mchakato wa kuzilipa fedha hizi kwa wakulima unaende
[20:04, 01/05/2020] Fadi: lea,'' alisema Myao.

Katibu tawala msaidizi huyo wa mkoa alisema uwepo wa korosho zisizo na ubora kwenye maghala makuu(Reject) katika msimu huo baadhi ya vyama vya msingi vilipeleka kwenye maghala makuu zisizo na ubora.

Kwahiyo kusababisha kutonunuliwa na zinaendelea kubaki kwenye maghala husika. Ambapo kilo 23f,188 hazikupokelewa, kati ya hizo katika ghala la Nangurukuru kilo 101,828 na BUCO kilo 131,360.

Myao pia alisema  kuharibika kwa barabara ya kutoka Nachingwea kwenda Liwale kutokana na mvua kumesababisha wanunuzi kushindwa kutoa na kusafirisha korosho kutoka katika ghala la Umoja. Hali inayosababisha baadhi ya korosho zilizotoka kwenye vyama vya msingi vya ushirika kuchelewa kuingia kwenye ghala kuu hilo.

Katika msimu wa 2019/ 2020 mkoa wa Lindi ulikadiria kukusanya na kuuza  kilo 80,000,000 za korosho. Ambapo hadi kufikia tarehe 20.04.2020 zilikusanywa kilo 59,970,00 nazimeuzwa kilo 58,757,222 zenye thamani ya shilingi 153,411,841,798.00.

'' Kati ya fedha hizo  jumla ya tsh 138,123,737,178.00 zimelipwa kwa wakulima,'' aliongeza kusema Myao.

 Juhudi za kuwapata maofisa wa kampuni za 3B&D Holdings Co, Ltd na Jaharin Commodities Ltd ili wathibitishe yale yalielezwa kuhusu kampuni zao zinaendelea.

Kikao hicho cha tathimini ya ununuzi wa korosho msimu wa 2019 na maandalizi ya ununuzi wa ufuta msimu huu kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi iliyopo mjini Lindi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...