Akina mama eneo la Murang'a nchini Kenya wamelalamikia kuhusu kuhangaishwa na genge la wezi sugu ambao wanawapora chupi kila uchao.
Wanasema sasa hawapumuia kwani chupi zao zinasakwa sana na wezi ambapo kundi hilo la wezi limekuwa likivamia makazi yao na kuanua nguzo hizo kwenye kamba.
Kwenye ripoti na gazeti la People Daily, kina mama hao wamesema sasa wamelazimika kuchunga nguo hizo za ndani kama dhahabu.
"Tumeshtuka kwa sababu hawa wezi wanaiba tu suruali za kina mama na kuwacha za wazee. Sasa ata hatujui wasichana wetu watavaa nini shule zikifunguliwa," mama mmoja amesema.
Aidha kina mama hao wanasema huenda chupi hizo zinatumika kutengeneza barakoa na kisha kuuziwa wakazi.
"Naskia wanatumia chupi zetu kutengeneza barakoa. Chupi moja inatengeneza maski mbili ... kwa suruali zile kubwa, naskia eti wanatumia kuunda maski tano," mkazi aliongeza. Eneo hilo liligonga vichwa vya habari awali baada ya wakazi kuonekana wamevalia chupi kama maski. Walikuwa wameuziwa chupi hizo aina ya thong kama barakoa bila ya kujua na ikawa kicheko kwa waliofahamu yaliyokuwa yamefanyika",wanaeleza.