Saturday, May 2, 2020
Spika Ndugai afunguka kuhusu agizo la Mbowe kwa wabunge wa CHADEMA
Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kuwa kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, haimbabaishi na chochote kwa kuwa kila jambo lao wanaweka upinzani na Wabunge ni timu moja na yeye ameamrisha timu yake tu bila kushirikisha wenzake, hivyo Wabunge wa CCM watabaki na kuendeshesha Bunge.
Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 2, 2020, wakati akizungumza , na kuongeza kuwa agizo la Mbowe kwa Wabunge wake wamelipokea kwa mikono miwili, na kwamba amekuwa ni kiongozi wa kuamrisha tu na ndiyo maana wanachama wake wengi wanahama, na kuongeza kuwa janga la Corona ni la Dunia nzima na hakuna ambaye anapenda kuona watu wakifa.
"Sisi halitushangazi hawa wenzetu kila jambo lazima waweke upinzani hata kama ni janga, Wabunge ni timu moja hauwezi kuamrisha tu wachezaji wako kwamba tokeni bila kuzungumza na wenzako, Wabunge wa CHADEMA wana bahati mbaya sana kazi yao ni kuamrishwa tu kama watoto wa Primary vile na wanalalamika kimya kimya sana kwangu" amesema Spika Ndugai.
Aidha Spika Ndugai alizungumzia suala la kupokea ushauri wa Mbowe "Wala siko tayari tena, yeye aendelee tu na Methodology zake kwa sababu muda mfupi ujao tutamaliza Bunge kwa kuzingatia tatizo la Corona na toka tumeanza tumezingatia na tumebadilisha mambo mengi sana".
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...