Sunday, April 26, 2020

Ulaya yataka usitishaji wa mapigano Libya

Mawaziri wa Mambo ya nchi za kigeni wa Ujerumani, Ufaransa, Italia pamoja na Umoja wa Ulaya wametoa tamko la pamoja linaloelezea wasiwasi wao kuhusiana na ongezeko la mapigano nchini Libya.

Katika taarifa ya pamoja, wamezitaka pande hasimu nchini Libya kurejea kwenye meza ya mazungumzo na kutafuta makubaliano ya uhakika ya usitishaji mapigano.

Viongozi hao wametilia mkazo umuhimu wa kuwepo utulivu wa uhakika katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na wakati Libya inaendelea kukabiliana na mlipuko wa viruis vya corona.

 Hivi karibuni mapigano yameongezeka kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli licha ya kutiwa saini mkataba wa kusitisha mapigano mnamo mwezi Januari.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...