Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan amewataka masheha wa mkoa huo kusimamizi kwa karibu vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuimarisha ustawi wa jamii wakati taifa likipambana na maambukizi ya maradhi ya corona.
Akizungumza kwa wakati tofauti katika vikao vilichowashirikisha viongozi wa wilaya, manispaa na jeshi la polisi, Hassan alisema vikundi vya ulinzi shirikishi vinapaswa kuendesha shughuli zao vizuri kama ilivyo azma ya serikali.
Alisema serikali imeanzisha vikundi hivyo kwa nia nzuri ya kuwashirikisha wananchi kushirikianan na jeshi la polisi katika kulinda usalalma wao na mali zao hivyo sio busara kuona wanatumia vibaya nafasi hiyo.
"Serikali imekuwa na dhamira njema kuruhusu kuanzisha ulinzi shirikishi kwa vile vikosi vyetu vya ulinzi pekee visingetosheleza kusimamia usalama katika maeneo yote na muda wote," alisema Hassan.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi hao kushirikiana kuandaa utaratibu maalum utakaohusisha upatikanaji wa sare na vitambulisho vya kuwatambua pamoja na kuwapatia mafunzo ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Akizungumzia kuhusu kukabiliana na maambukizi ya maradhi ya corona, Mkuu huyo wa mkoa aliwataka Masheha kupita nyumba kwa nyumba kutoa elimu juu ya madhara hayo huku akiwataka kutoa taarifa za wageni wanaoingia katika shehia zao.
Katika hatua nyengine Hassan aliwataka viongozi wa mabaraza ya Manispaa mkoani humo kushirikiana na jeshi la polisi kutambua vituo vya vyombo vya moto ikiwemo pikipiki umaarufu kama bodaboda zilizomo katika manispaa zao ili kupunguza vitendo vya uhalifu na ajali za mara kwa mara.
Mapema akizungumza katika mkutano huo Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Awadh Juma Ali alisema jeshi la polisi liwachukulie hatua baadhi ya vikundi vya watu vinavyojihusisha na matendo yauhalifu katika mkoa huo.
Aidha aliwaomba masheha kushirikiana na jeshi la polisi kubaini vikundi vinavyojishughulisha na maswala ya uhalifu katika maeneo yao ili vidhibitiwe kwa kuchukuliwa hatua.
Alisema jeshi la polisi litahakikisha linasimamia kwa karibu maelekezo, miongozo na maagizo ya serikali kuu kuhusu kutokuwepo kwa mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na kuwataka wananchi kufuata maelekezo hayo sambamba na kutii sheria bila ya shuruti.
Wakizungumza mara baada ya mkutano huo, baadhi ya viongozi walioshiriki vikao hivyo waliahidi kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yaliyotolewa na kuwataka wananchi kutoa mashirikiano ili kuhakikisha mapambano ya maambukizi ya maradhi ya corona yanafanikiwa.
Source
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
