Mbunge wa Mtama, @nape_nnauye, leo alipata nafasi kuchangia huko Bungeni. Pamoja na mengine, Nape alisema "Rais Magufuli hakuteuliwa bahati mbaya tuliona ataweza kutekeleza kazi tuliyompa na nina hakika #CCM ikifanya tathmini leo, lazima itampa tena nafasi ya kuendeleza kazi ambayo ilimkabidhi pamoja na kazi nyingine"
Nape aliongeza "Ninaipongeza sana Serikali kwa kazi nzuri iliyofanya, ninaamini kuwa chama changu kitasimama na kitampa tena nafasi Rais Dkt Magufuli, kuendelea kuongoza kwa miaka mitano mingine na wananchi nao watasimama naye."