Tuesday, April 14, 2020

Iran: Vifo vinavyotokana na virusi vyapungua

Iran imesema leo kuwa idadi ya matu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa virusi vya corona imeshuka kwa alama mbili kwa mara ya kwanza katika kipindi cha mwezi mmoja.

Msemaji wa wizara ya afya ya Iran Kianoush Jahanpour amesema vifo 98 vya ugonjwa wa covid-19 vimerikodiwa katika muda wa masaa 24, na kufikisha jumla ya watu waliofariki kuwa 4,683.

 Jahanpour amesema watu wengine 1,574 wamegunduliwa kuambukizwa virusi hivyo, na kufanya jumla ya visa vya maambukizi nchini Iran kuwa 74,877.Ameongeza hata hivyo kwamba watu 48,129 waliokuwa wamelazwa hospitalini wamepona na kuruhusiwa.

Serikali ya rais Hassan Rouhani imepambana kudhibiti mripuko huo ulioanza karibu miezi miwili iliyopita.
Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...