Sunday, April 12, 2020
Baada ya Mrembo Nicole Kumpa TAMU Harmonize..Sarah Ajirudi na Kukubali Yaishe
Moshi mweupe! Mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul 'Harmonize', Sarah Michelotti amefufua matumani ya wawili hao kurudiana kufuatia kitendo chake cha kujirudi na kumtumia mwenzi wake huyo ujumbe mtamu wa kimahaba.
Sarah ambaye ni raia wa Italia na Harmonize au Harmo, wiki iliyopita waliingia kwenye mgogo mkubwa wa kimapenzi kwa tuhuma za usaliti.
Sarah alidaiwa kumtuhumu Harmo kusaliti penzi lao kwa kulala na video queen matata Bongo, Nicole Joyce Berry ambaye amemtumia kwenye video yake ya Wimbo wa Bedroom.
Sarah alidaiwa kutinga nyumbani kwa Nicole maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar kisha kufanya fujo akimtuhumu mrembo huyo kutembea na Harmo.
Nicole alidaiwa kumpa 'tamu' bosi huyo wa Lebo ya Konde Music Worldwide walipokuwa wakishuti video ya Wimbo wa Bedroom.Hata hivyo, inaonekana mambo yameanza kukaa vizuri baada ya Sarah kumaliza hasira zake na kuanza kufuta zile tetesi kwamba wameachana.
Kupitia Insta Story kwenye ukurasa wake wa Instagram, Sarah alitupia picha ya Harmo akipafomu jukwaani na kuandika;"Mume gharama zaidi wa moyo wangu.
Wakati wote hukosei baby harmonize_tz"Pamoja na hayo, lakini bado wawili hao hawajarejesha ufuasi wa kila mmoja kwenye kurasa zao za Instagram baada ya kuondoana wiki iliyopita hivyo kuendeleza sintofahamu juu ya uhusiano wao.
Stori:NEEMA ADRIAN, Ijuma
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
