Friday, March 27, 2020
Wizara ya Elimu imetoa elimu kwa wafanya kazi wake
Na Thabit Madai
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amesema Wizara yake imeamua kuwapatia Elimu wafanyakazi wake juu ya kujikinga na virusi vya korona.
Amesema kutokana na kuenea kwa kasi kwa virusi hivyo duniani ipo haja ya kuwaelimisha watendaji wa Wizara hiyo ili waweze kufanyakazi kwa umakini.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu ya Afya katika viwanja vya Wizara hiyo Mazizini Mjini Unguja Mhe Simai amewataka wafanyakazi hao kuwa makini pamoja na kuifanyia kazi elimu waliyoipata na kuwa mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wengine ili kuweza kujikinga na maradhi hayo.
Nae Afisa mahusiano kutoka kitengo Cha Elimu ya Afya Bwana Ahmed Mohamed amesema virusi vya ugonjwa wa Korona husambaa haraka, hivyo ni vizuri kwa kila mmoja kuchukua tahadhari ya hali ya juu ili kuepuka maambukizo ya virusi vya korona.
Amesema virusi husambaa kwa kushikana au kugusa sehemu za vitasa, funguo, ambavyo alieathirika aliaacha virusi huku maambukizi,na dalili zake ni kupata homa Kali na kifua kikavu, kuumwa na kichwa Sana na machofu mwilini.
Aidha amesema Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi kwa kila raia atakaeingia nchini kutoka nchi iliopata maambukizi, lazima awekwe kwenye Maandalizi Maalum kwa muda wa siku kumi na nne.
Nao Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu Zanzibar wameishukuru Wizara yao kwa hatua waliochukua viongozi wao kwa kuwapa Elimu watendaji wake, ambayo imewasaidia kujua Kinga na athari za virusi vya korona.
Aidha wametoa wito kwa wazazi kuwasimamia watoto wao juu ya kutozurura ovyo na badala yake kujisomea majumbani mwao ili kuwaepusha na maambukizi hayo.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...