Nyota mkongwe wa muziki wa Afro-jazz Manu Dibango, amefariki dunia leo baada ya kuambukizwa virusi vya vipya corona.
Wawakilishi wake wamesema mwanamuziki huyo nguli raia wa Cameroon amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya eneo la mji wa Paris, Ufaransa.
Dibango, aliyekuwa na umri wa miaka 86, na anayefahamika kwa kibao cha "Soul Makossa", cha mwaka wa 1972, ni mmoja kati ya nyota wa kwanza wa kimataifa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19.
Ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook umesema kuwa mazishi yake yatafanyika kwa usiri mkubwa, na kwamba hafla ya kumbukumbuka itapangwa katika wakati muafaka.
Dibango alitengeneza muziki wa Afro jazz na pia kuuchanganya na muziki wa kitamaduni wa Cameroon.