Tuesday, March 24, 2020

Mvua zasitisha mawasiliano Ruvuma

Wananchi na wasafiri wanaotumia barabara kuu ya Likuyufusi -Mkenda ambayo inaunganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji mkoani Ruvuma wako katika wasiwasi mkubwa wa kukosa mahitaji ya msingi kama huduma za afya ,usafirishaji wa mazao baada ya daraja la mto Nakawale kulika pembeni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Baadhi wa wananchi wa kijiji cha Nakawale kata ya Mhukuru Halmashauri ya wilaya ya Songea wanasema mvua hiyo ilinyesha kwa siku mbili mfululizo na kufunika daraja la mto Nakawale hali iliyopelekea pembeni mwa daraja ilo kulika na kusababishaa mgari kushindwa kupita kwa hofu ya daraja kukatika.

Romani Mbukini ni Mhandisi wa matengenezo kutoka wakala wa barabara nchini Tanroads Ruvuma anasema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wamekuja kufanya tathimini na ndani ya siku mbili mawasiliano yatarejea.

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya anatoa maagizo kwa Tanroad kuhakkisha mawasiliano yanarejea kwa wananchi kutokana na umuhimu wa barabara hiyo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...