Friday, February 7, 2020
Mwamuzi Aliyeruhusu Goli la Kagera Afungiwa Miaka Mitatu
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepitia mwenendo wa matukio ya ligi na kufanya maamuzi mbalimbali ikiwemo utoaji adhabu kwa wahusika.
Katika kikao hicho cha Februari 03, 2020, kamati imeridhia kumfungia miaka mitatu mwamuzi msadizi namba mbili wa mchezo namba 150: kati ya Simba SC (3-2) Namungo FC Kassim Safisha kwa kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea (offside) katika mechi hiyo.
Wakati huo huo Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa barua ya kukumbushwa kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika mechi namba 157 iliyochezwa Januari 30, 2020 kati ya Azam FC (1-1) Mtibwa FC kwenye Uwanja wa Taifa.
Vile vile katika mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya makamishina kutokana na kutoa taarifa yenye mapungufu huku adhabu hiyo ikitafsiriwa kulingana na kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti kamishina wa mchezo.
Katika mechi namba 75A kati ya Friends Rangers (0-1) Dodoma FC, Kiongozi wa Klabu ya Friends Rangers Heri Chibakasa amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kupigana na mashabiki wa timu pinzani.
Aidha TPLB imetoa adhabu kwa Mwamuzi Salum Mkole ambaye amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kuonesha udhaifu katika usahihi wa kutoa kadi katika mechi namba 29A iliyochezwa Januari 31, 2020 kati ya Dar City Fc (1-0) African Sports, katika dimba la Uhuru.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...