Thursday, February 27, 2020

Mambo 6 ambayo Mjasiriamali anatakiwa kuyafanya kila siku


Kati ya kitu ambacho kila mjasiriamali mwenye nia ya kufanikiwa anacho ni kule kutaka kuona anakifikia mafanikio makubwa ya kibiashara. Lakini pamoja na kuwa na nia hiyo ya kufikia mafanikio hayo, mjasiriamali huyu hawezi kufanikiwa mpaka ajue mambo ya msingi yanayoweza kumsaidia kufanikiwa na kuyafanya karibu kila siku.

Kwa mjasiriamali yoyote atakayeelewa mambo hayo itamsaidia sana kuweza kufikia mafanikio makubwa anayohitaji. Kwa kujifunza kupitia makala haya, itakuonyesha mambo ya wazi ambayo unatakiwa kuyajua kama mjasiriamali na kuyafanya kila wakati ili kuweza kufanikiwa. Sasa twende pamoja kuweza kujifunza mambo unayotakiwa kuyazingatia kila siku katika safari yako ya mafanikio.

1. Panga siku yako mapema.
Ni rahisi sana siku yako kuwa ya mafanikio ikiwa utaipangilia mapema. Ni vizuri ukaipangilia siku yako mapema ikiwezekana siku moja kabla ili kuweza kujua ni kitu gani utakachokifanya kesho. Hiyo itakusaidia kuweka malengo na kupanga mikakati muhimu ya kutekeleza mapema kichwani mwako kwanza.

Kwa mfano usiku kabla hujalala andika kwenye kitabu chako ni nini utachokwenda kufanya kesho. Kwa kufanya hivyo kila siku itakusaidia kufanya mambo mengi kwa urahisi na bila kupoteza muda hovyo. Acha kulala na kuamka kiholela. Unaweza ukaona ni jambo kama dogo, lakini lina msaada mkubwa sana katika safari yako ya mafanikio na ni muhimu kufannya hivi kila siku.

2. Amka asubuhi na mapema.
Siku zote jifunze kuamka asubuhi na mapema. Unapoamka asubuhi na mapema inakusaidia sana kukamilisha zile kazi ngumu ambazo unatakiwa uzifanye kwa siku husika. Kuamka asubuhi na mapema ni muhimu hiyo yote ni kwa sababu akili yako inakuwa bado na nguvu kubwa ya kutenda mambo mengi na kwa ufanisi mkubwa bila kuchoka.

Unaweza ukaamka asubuhi na mapema ukajisomea. Kama wewe ni mwandishi unaweza ukaamka asubuhi na mapema ukaandika au ukapitia malengo yako. Kwa kuamka asubuhi na mapema itakusaidia sana kama mjasiriamali kukufanikisha kwa sababu mipango yako mingi unaweza ukaifanya asubuhi na mapema hata kabla jua halijazama.

3. Anza siku yako kwa kuwa chanya na maliza ukiwa chanya.
Amka asubuhi kwa kujifunza kuwa chanya. Hiyo itakuwa rahisi kwako ikiwa utajisomea kitabu au utasikiliza kitabu cha sauti kupitia simu au redio. Unapoianza siku yako ukiwa chanya utaifanya siku yako iwe nzuri zaidi. Mambo yako mengi utayafanya kwa hamasa kubwa. Kitu pekee kitakachokufanya uwe hivyo ni kwa sababu uliianza siku yako ukiwa chanya.

Lakini si hivyo tu, kama ulivyoanza siku yako chanya ndivyo unatakiwa uimalize kwa namna hiyo. Imalize siku yako kwa kujikumbushia tena malengo yako. Imalize siku yako kwa kujisomea kitabu cha mafanikio hata kwa dakika kumi na tano. Hivi ndivyo unavyoweza ukawa chanya kwa siku yote na itakusaidaia kuwa mjasiriamali wa mafanikio.

4. Tunza na thamini muda wako.
Muda ni kitu cha thamani sana kwa mjasiriamali yoyote. Muda ndio unaotufanya tufanikiwe ama tusifanikiwe. Matumizi ya muda sahihi yanahitajika sana katika kila eneo la maisha yetu kuliko wengi wanavyofikiri. Hivyo kwa maana hiyo ni muhimu sana kuthamini muda tulionao na kufanya yale yaliyo ya muhimu kwetu.

Kama ulikuwa ni mtu wa kupoteza muda, achana na hiyo tabia mara moja. Sasa unatakiwa kuishi maisha ya kimafanikio kwa kuthamni na kutunza muda wako sana. Usikubali mtu yoyote akakupotezea muda wako. Wajasirimali wengi wenye mafanikio wanatunza sana muda wao. Kama lengo ni kuwa mjasirimali wa mafanikio ni vyema kujifunza kutunza na kuthamini muda sana kila siku.

5. Jiwekee lengo la kusonga mbele kila siku.
Mjasiriamali mwenye mafanikio lengo lake kubwa ni kusonga mbele. Haijalishi unakutana na nini? Lakini ukiwa kama mjasirimali unayetaka kufanikiwa thamani kuendelea mbele. Acha kuganda na kung'ang'ania sehemu moja ulipo  hiyo haitakusaidia sana. Kikubwa uwe mtu wa kusogea hatua kwa hatua kila siku.

Najua kuna wakati tunakutana na changomoto nyingi sana. Pamoja na changamoo hizo zichukulie kama ngazi ya kukupandisha kwenye mafanikio yako. Lakini ikiwa utakubali kukaa chini nakutulia basi elewa wewe mwenyewe utakuwa umeamua kuyapoteza maisha yako bila kujua. Tambua kusonga mbele liwe ndilo lengo lako la kwanza kama mjasiriamali unayetaka mafanikio makubwa.

6. Jifunze kila siku.
Yafanye maisha yako kila siku yawe shule. Kila unachopitia iwe changamoto au kile kizuri unachokiona kutoka kwa watu wengine kifanye kiwe sehemu ya darasa kwako la kukutoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Andika yale mambo ya msingi ambayo unaweza ukawa umejifunza na kisha yafanyie kazi kila siku. Hapo itakusaidia sana kuwa mjasiriamali wa mafanikio.

Naamini kwa kujifunza mambo hayo, yatakuwa msaada kwako wewe kama mjasiriamali kuweza kufanikiwa kwa kile unachokifanya katika maisha yako. Kumbuka kuchukua hatua na kufanyia kazi kile ulichojifunza.

Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,

Vijue vikwazo vikuu vya mafanikio yako

Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako.  Watu wengi tumekuwa tukijiambia maneno ambayo kimsingi yamekuwa ni kikwazo kikubwa sana cha kuweza kufanikiwa kwa namna moja ama nyingine.

Vifutavyo ndivyo vikwazo ambavyo huviweka wenyewe katika suala la mafanikio:

Sina muda wa kutosha
Hili ni swala ambalo watu wengi hulalamikia kila siku kuwa hawana muda kutosha. Fahamu kuwa hakuna binadamu duniani mwenye zaidi ya saa 24. Hivyo kama unapata muda wa kutumia mitandao ya kijamii, kucheza michezo ya kompyuta au kuchati kwa simu basi una muda mwingi mno kuliko unavyofikiri.

Badilisha fikra zako leo, jifunze kutumia muda wako vyema ukijiwekea vipaumbele na malengo ya kukamilisha kila siku.

Ni vigumu kuanza
Ni kweli kuwa hata wahenga walisema "mwanzo ni mgumu" lakini hilo sio kanuni. Kila mtu duniani angewaza mwanzo ni mgumu nafikiri tungekuwa bado kwenye zama za ujima.

Jifunze kwa waliofanikiwa, walianzaje? walizikabili vipi changamoto? Siku zote jifunze kuona mafanikio kabla ya changamoto, hili litakupa hamasa na kiu ya kufanya bidii hata kuzishinda changamoto.

Inasikitisha kuona kuwa watu wengi hawafikii malengo yao kwa sababu ya mambo wanayojiambia au kujiwazia wenyewe. Ninakuhamasisha kuwa, kama unapumua basi unaweza kufanikiwa. Inaweza kuchukua muda lakini ukiamua unaweza.

Source

Angalia picha :WAZIRI KAIRUKI AONGOZA MKUTANO MKUBWA WA MASHAURINO KATI YA SERIKALI,WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI MKOA WA SHINYANGA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki ameongoza Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ili kusikilizwa na kupata ufumbuzi wa changamoto katika maeneo yao ya uwekezaji na biashara kwa lengo la kuboresha biashara na uwekezaji ili kuongeza wigo wa ajira kwa vijana na kulipa kodi kwa hiari.

Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Februari 26,2020 katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri kutoka Wizara nane ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Wizara ya Fedha na Mipango, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Madini. 

Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki alieleza namna Serikali ilivyoendelea na jitihada za kuhakikisha uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya uwezeshaji biashara (Business Facilitation Acts).

Mhe. Kairuki alisema uwepo wa mikutano hiyo inaongeza hamasa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kueleza kero wanazokabiliana nazo pamoja na kupatiwa majibu ya papo kwa hapo na Mawaziri wa Sekta husika.

"Mikutano imeibua hoja muhimu zilizopatiwa ufumbuzi na mawaziri wa sekta mbalimbali niwatoe shaka Serikali itaendelea kuwaunga mkono na ni vyema mkaendelea kufuata sheria na kanuni zilizopo katika kuwekeza kwenu,"alisisitiza Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wanapokuwa na migogoro wasisite kuwasiliana na serikali ili kuitatua na kuepuka kusababisha migogoro kuwa mikubwa.

Alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kutenga jumla ya hekta 200 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo na hekta 640 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vikubwa katika eneo la Bukondamoyo kata ya Zongomela wilayani Kahama ambalo tayari serikali imetumia shilingi 809,400,000/= kwa ajili ya kuliwekea miundombinu wezeshi ikiwemo barabara,umeme na maji.

"Kuhusu suala la Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli nitalifuatilia kwa ukaribu kwani limelalamikiwa kuwa changamoto kwa wafanyabiashara",alisema Kairuki.

Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega aliwahakikishia wafugaji wa samaki kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuwawezesha wafugaji kufuga samaki na kueleza kuwa, mabwawa ya samaki yameongezaka kutokana na jitihada zilizopo na kueleza namna Serikali inavyoendelea kudhibiti uvuvi haramu Baharini na kwenye Maziwa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo namna Wizara yake ilivyojipanga kuondoa changamoto za gharama kubwa za mikopo katika benki pamoja na suala la utitiri wa kodi baada ya kulalamikiwa na wafanyabiashala hao.

"Nimewafurahia wana Shinyanga kwa uwazi wenu wa kujieleza vizuri, niwahakikishie kuwa,mwisho wa malalaiko yenu haupo mbali tutahakikisha sekta ya fedha inatatua kero zenu na kushughulikia upatikanaji wa mikopo na kwa gharama zinazoeleweka,"alieleza Dkt. Kijaji.

Kijaji alisema serikali itayafanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara ikiwemo tozo nyingi huku akisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kulipa kodi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alisema mkoa wa Shinyanga umefanya jitihada kubwa ya kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambapo hadi sasa kuna jumla ya Viwanda 729 kati ya hivyo,Viwanda Vikubwa ni 13,viwanda vya kati 11 na viwanda vidogo 705 ambavyo vimeajiri wafanyakazi 10,150. 

Telack alisema mkoa wa Shinyanga umetenga jumla ya hekta 20,289.25 kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara,kilimo na viwanda kati ya hekta hizo, Halmashauri ya Mji wa Kahama imetenga hekta 2,000,halmashauri ya Shinyanga 5,560, Ushetu 2,110,Kishapu 10,361.70 na Msalala hekta 257.53. 

Hata hivyo kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaozaliwa na wanaohamia Telack alisema hali hiyo imesababisha uhitaji wa ujenzi wa shule,vituo vya huduma za afya,ujenzi wa nyumba za kulala wageni na kadhalika. 

"Serikali imetengeneza mazingira wezeshi kwa wazawa kuingia kwenye biashara ya Madini ya almasi kwa kuuelekeza Mgodi wa Almasi wa Mwadui (WDL) kuuza asilimia 5 ya almasi inayozalishwa ndani ya soko la ndani kwa njia ya mnada na uuzaji wa kawaida.Natoa rai kwa wafanyabiashara wote kuchangamkia fursa hii ili baadaye almasi yote inayozalishwa iuzwe ndani ya mkoa wetu na kuongeza ukuaji wa wa uchumi wa mkoa",alisema Telack.

Kwa Upande wake,Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu Dk. Zumbi Musiba akimwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick, alisema Barrick inashukuru kwa fursa ya kufadhili Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ili kushirikiana na serikali kuchangia katika kuendeleza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.

"Wengi wa washiriki wa mkutano huo ni wadau wa Kampuni ya Barrick hivyo hiyo ni fursa nzuri ya kusikia wanakabiliwa na changamoto zipi ili kwa pamoja tuweze kuzitafutia ufumbuzi",alisema Dk. Musiba.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Wafanyabiashara na Wawekezaji zaidi ya 560 umeandaliwa na Kamati Tendaji ya Baraza la Biashara mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) kwa ufadhili wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick, Benki ya CRDB,NMB, TPB na NBC. 
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 26,2020 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiongoza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu  Dk. Zumbi Musiba akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe, Jasinta Mboneko ( wa kwanza kulia) wakiwa ukumbini.
Meza kuu wakifuatilia matukio ukumbini.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Wadau wakiwa katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dk. Meshack Kulwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dk. Meshack Kulwa akiteja jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia).
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa  Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali wakiwa ukumbini.

Wadau wakiwa katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkutano unaendelea.
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constatine  Kanyasu akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angellina Mabula akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
 Wadau wakiwa ukumbini.
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Karena Hotel,Josephine Wambura akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea.
Mwenyekiti wa Shirikio la Wamiliki wa Shule Binafsi mkoa wa Shinyanga, Jackton Koyi akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kahama Plastic Investment (T) Limited Kazimoto Leonard akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa dini wakifuatilia mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Meneja wa Benki ya TPB mkoa wa Shinyanga Jumanne Wagana akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Sospeter Magese akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Meneja wa Benki ya NBC mkoa wa Shinyanga Happiness Kizigira akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Dk. Seif Said kutoka Kahama akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Katibu wa SHIREMA, Gregory Kibusi akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mfanyabiashara Edna Catherine Wanna akizungumza katika mkutano huo.
Wadau wakiwa ukumbini.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya amani mkoa wa Shinyanga Sheikh Khamis Balisusa akiomba dua kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini mashariki ya Ziwa Victoria, Dk. Emmanuel Joseph Makala akiomba kabla ya kuanza Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...