Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Jamila Muga (Julia),akionyesha simu janja na ya gharama nafuu ya SMARTA iliyozinduliwa na Zantel mjini Zanzibar. Simu hii inayonunuliwa ikiwa na GB 12 intaneti inayowezesha matumizi ya mwaka mzima inapatikana kwa shilingi 39,999/- nchini pote. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Zantel
**
Katika jitihada zake za kuongeza wigo wa watumiaji wa simu janja nchini Tanzania, Zantel imezindua simu janja yenye uwezo wa 4G na gharama nafuu sana sokoni ijulikanayo kama SMARTA.
Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Jamillah Muga, alisema simu iliyozinduliwa imetengenezwa kwa teknojia zinazowezesha matumizi ya programu za simu janja zinazowezesha kupata programu za kuelimisha na kuburudisha kama vile, WhatsApp, Facebook, YouTube, Google na inapatikana kwa bei nafuu ya shilingi 39,999/-.
Alisema simu ya SMARTA ni aina mpya ya simu katika soko la Tanzania inayowezesha kuongeza idadi ya watumiaji wa simu janja nchini kote na kuleta mabadiliko ya kidigitali kwenye jamii.
"Tumezindua simu aina ya SMARTA katika soko kuwezesha wananchi wengi kumudu kumiliki simu janja sambamba na kuwapatia fursa ya kufurahia maisha ya kidigitali kupitia mtandao wa 4G+ wa Zantel". Alisema Muga.
Muga, alisema kuanzia sasa simu janja zijulikazo kama SMARTA zinapatikana katika maduka yote ya Zantel yaliyopo Pemba, Unguja, na Tanzania bara na zinanunuliwa zikiwa tayari zimeunganishwa na intaneti ya bure yenye GB 12 itakayowezesha mteja kuitumia kwa kipindi cha miezi 12.
Mkuu wa Zantel Zanzibar,Mohammed Mussa Buacha, alisema kuzinduliwa kwa simu mpya za SMARTA ni moja ya mkakati wa Zantel kuleta mapinduzi ya kidigitali na kuwezesha kupatikana teknolojia za kisasa kwa gharama nafuu nchini kote. Alisema Zantel inaamini kuwepo kwa bidhaa za kisasa kwa matumizi ya huduma za kidigitali kunabadilisha maisha ya wananchi kuwa bora.
''Kupitia mapinduzi ya kidigitali yanawezesha kupata elimu, taarifa za afya, burudani, huduma za kifedha na kwenye intaneti inawezesha kujua mambo mbalimbali yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku. Dira ya Zantel ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kidigitali kwa manufaa ya wateja wetu wapya na wa zamani". alisisitiza Mussa.
Alisema kupatikana kwa simu za gharama nafuu za SMARTA, ni suluhisho la kuwezesha watanzania wengi kuweza kumudu kumiliki simu janja nchini na kuwezesha kuendeleza matumizi ya huduma za kidigitali Zanzibar "Kuanzia sasa Watanzania hawana sababu ya kuwa na vikwazo wanapotaka kununua simu janja".
Zantel imekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika ubunifu kwendana na ongezeko la watumiaji wa huduma za data na kuunganishwa kwenye intaneti yenye kasi kubwa ambapo ili wengi wafurahie huduma hizo kunatakiwa kuwepo simu janja za gharama nafuu.